MPEPE333
Member
- Nov 28, 2011
- 31
- 21
Habari wana jamvi, poleni na majukumu ya kila siku katika kulijenga taifa letu.
Naomba niende kwenye mada hapo juu, ni hivi:
Shule ya Tunduru Jamhuri Academy ni shule ya serikali inayosajiliwa kama English medium na inaendeshwa kwa michango ya wazazi tangu kuanzishwa kwake, shule hii tangu ilipoanzishwa imeweza kutoa fursa hata kwa familia za kipato cha kawaida kuwezesha watoto wao kuonja angalau ladha ya private schools ambazo wasingeweza kumudu gharama, lakini kupitia shule hii wazazi wanafurahia kuwasikia watoto wao wanapata uelewa wa lugha ua kiingereza ambayo ndo msingi mkubwa wanapoingia o level
Kilichonisukuma kuleta hapa uzi huu ni maazimio ya kikao kilichoketi tarehe 21.12.2024 ambacho kilihudhuriwa na wazazi wachache sababu kilikuwa ni cha ghafla na ulikuwa msimu wa likizo, maazimio ya kikao hicho ni kwamba gharama ya usafiri iwe ni lazima kwa watoto wote, bila kujali unataka hiyo huduma au lah, bahati mbaya ni kwamba hiyo hiyo huduma ya usafiri inatolewa na mtu binafsi na sio mali ya shule. Hili suala limeleta taharuki kwa wazazi ambao walizoea kujitegemea usafiri ambao wanaumudu, na wengine watoto wao wanaishi jirani na shule lakini wanaambiwa ni lazima walipie laki mbili 200,000 kwa mwaka, kama una watoto watatu ni laki sita kwa mwaka
Wazazi walioonesha kutokukubaliana na hilo jambo hawajapewa nafasi ya kusikilizwa, mwalimu mkuu amekuwa mkali sana ukihoji hilo jambo, anasema anasimamia maazimio ya wazazi, na usipokubaliana nae anasema anaingia kwenye mfumo na anamtoa mtoto wako kwenda shule za kawaida.
Hilo suala la kuwafukuza watoto ameishaaanza kulitekeleza na anasema hata uende kwa Mkurugenzi au Afisa Elimu hawana cha kunifanya. Hili ni kweli maana wazazi wote waliojaribu kwenda kwa afisa elimu na mkurugenzi hawajapata msaada wowote.
Ndugu msomaji jaribu kuvaa viatu vya hawa wazazi wa hali ya chini wanafukuzwa watoto wao, manaake mzazi aanze upya kushona sare, mtoto aanze kupambana na mtaala mwingine ghafla, mtoto aanze kutembea umbali mrefu kuitafuta shule nyingine wakati anapoishi pana shule ya umma kisa tuu mzazi ameshindwa kumudu gharama ya usafiri ambao sio hitaji lake
Hii pesa inayochangishwa kwa wazazi ambao watoto wao hawapandi gari inaenda wapi? mamlaka ya mkuu wa shule kumwondoa mwanafunzi kwenye mfumo bila makubaliano na mzazi yanatoka wapi? Kwanini maslahi ya mwenye gari yanapewa kipaumbele kuliko maisha ya watoto? Mkuu wa shule anakaa na pesa kwenye droo yake, akimtoa mtoto wako kwenye mfumo anakupatia na chenji yako iliyobaki katika michango uliyokuwa umechangia
Michango halali na ya lazima ambayo kila mzazi yupo ridhaa ni ;
CHAKULA -,200,000
UJENZI - 100,000
GHARAMA YA UENDESHAJI SHULE NA POSHO YA WAALIMU WA KUJITOLEA - 200,000
Lakini sasa wanalazimisha kila mzazi alipe 700,000 .
imetengenezwa na fomu mpya isiyo na mchanganuo ili wazazi wasiweze kuhoji kwa tunalipia nini, wanasema gharama ya kusomesha mtoto katika shule hiyo kwasasa ada ni 700,000, hutaki tutamtoa mtoto wako kwenye mfumo.
Hii ni rushwa na ni ufisadi, tunaomba TAKUKURU TUNDURU, CAG, MDHIBITI UBORA ELIMU, NA VYOMBO VINGINE MLIANGALIE HILO JAMBO KWANI LINAKATISHA NDOTO ZA WATOTO WASIO NA HATIA KWASABABU TUU YA MASLAHI YA WACHACHE.
NAWASILISHA 🙏🙏🙏