Haruna Niyonzima Simba SC

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Afisa Habari wa klabu ya Simba amethibitisha kwamba Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa klabu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya zamani Yanga ambayo aliichezea hadi msimu uliopita.

Kulikuwa na tetesi nyingi kuanzia kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na hata kwa wadau mbalimbali kuhusu Niyonzima kusainiwa na Simba lakini klabu hiyo haikuthibitisha mapema hilo.

“Haruna Niyonzima ni mchezaji halali wa Simba tumeshamalizana nae, ameshamaliza mkataba na club aliyokuwa anaitumikia atakuja Simba. Anaweza akaenda South Africa kuungana na kikosi au anaweza kuja moja kwa moja Dar katika safari moja na Rayon Sport na atacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports siku ya Simba Day,” Haji S. Manara

Yanga tayari walishatoa taarifa mapema kwamba hawakufikia makubaliano na Niyonzima baada ya star huyo wa Rwanda kutaka dau kubwa ili aongeze mkataba mpya wa kubaki Yanga.

Kwa sasa Niyonzima yupo Rwanda mapumzikoni tangu kumalizika kwa ligi kuu Tanzania bara na kwa mujibu wa Manara, Niyonzima ataungana na wachezaji muda wowote wiki hii.
 
Mbona inaonekana kama Simba wanambembeleza sana Niyonzima? Maana tumeshuhudia wenzake wakimalizana kimaslahi na Simba wanawahi South Africa kuungana na wenzao. Yeye hata mazoezi hajafanya anaambiwa atacheza Simba Day! Asije akaigawa timu! Hii ni hatari kwa kweli.
 
Kuigawa timu kivipi, Niyo hakuwa anabembelezwa bali alikuwa bado ana mkataba Yanga, walikuwa wanategea mkataba uishe japo alishasaini kitambo. Kumtangaza kabla ya kuisha kwa mkataba Yanga ineleta shida.

Pili Simba Day ni siku ya kukitangaza kikosi hasa kuwatambulisha wachezaji wapya. Kwa hiyo hata angesaini leo kesho Simba Day angecheza tu coz ni kwa ajili yake na wenzake. Ligi inaanza tarehe 28/8 na 23/8 ngao ya hisani
 
Hii si breaking news mkuu,kitambo tu inajulikana huyo jamaa anaenda mkiani
Inajulikana kote duniani kuwa mtu akifikia umri wa kustaafu lazima ataelekea kwenye ofisi za mfuko wa hifadhi ya jamii. Mikia FC wanapumbazwa na usajili wa m'babu asiyeweza kucheza dkk 90 ilhali mambo klabuni yanatokota kati ya baraza la wadhamini na Bwana Moooo
 
Wamejaza majina tu,mwisho wa msimu ujao Yanga bingwa tena,watani wajiandae kwenda UN safari hii,maana FIFA washawachoka
 
Hawezi kugawa timu kaa kimya wewe, wala hajabembelezwa alikuwa na mkataba uloisha july 30 na pia alikuwa anasoma course ya ukocha,usijali mwanayanga atacheza tu vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawezi kugawa timu kaa kimya wewe, wala hajabembelezwa alikuwa na mkataba uloisha july 30 na pia alikuwa anasoma course ya ukocha,usijali mwanayanga atacheza tu vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
Kukaa kimya siwezi Mkuu lazima nitahadharishe ili mchukue hatua. By the way mkataba wa Niyonzima na Yanga uliisha tarehe 21 July 2017 na sio 30 July 2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…