Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 24
Siku hizi imekuwa fashion maharusi kuzunguka mabarabarani ili kujionyisha kwa umma baada ya harusi kufungwa.
Mizunguko hii inamaana gani lakini?
Mara nyingi husababisha msongamano wa magari barabarani.
jamani hizi harusi zinakera mno, hasa wenyeji wa arusha mtakubaliana na mimi, siku ya jumamosi kuna kua na foleni za hatari kisa harusi.. wanachukua barabara nzima, barabara zetu zenyewe finyu.. wengi wao ni kujionyesha tu, maana sio harusi tu mpaka ubarikio na vipaimara lazima wapite na matarumbeta mji mzima..
Ingependeza pia wanapotalikiana basi wafananye hivyo hivyo kujionyesha kuwa sasa tuameachana mitaani, na kwenye mabara bara!! Matarumbeta, na kila shamra shamra maana divorces need to be public as well
Masa
Siku hizi imekuwa fashion maharusi kuzunguka mabarabarani ili kujionyisha kwa umma baada ya harusi kufungwa.
Mizunguko hii inamaana gani lakini?
Mara nyingi husababisha msongamano wa magari barabarani.
Mimi sioni tatizo. Kwa wale wenye imani (dini) kama mimi, hii ni sikukuu ya kubwa katika maisha ya binadamu. Ni siku ambayo unakuwa umeweka agano mbele za Mungu kuwa na mwenzi wako mpaka kifo kitakapowatengenisha. Kwa kifupi ni siku kuu! Hapa kila mtu anapaswa kusheherekea kwa kila style. Ukiamua kupita jiji zima na matarumbeta, au ukiamua kwenda beach (kipindi kabla hazijafungwa) ni katika shamrashamra za kusheherekea. The public has to know bwana. Kama hukubahatika kufanya hivyo pole sana.
Ingependeza pia wanapotalikiana basi wafananye hivyo hivyo kujionyesha kuwa sasa tuameachana mitaani, na kwenye mabara bara!! Matarumbeta, na kila shamra shamra maana divorces need to be public as well
Masa
Waacheni wajitanue. Inawakera "in moral terms" lakini hamna hoja ya msingi kupinga hizo sherehe.
Siku hizi imekuwa fashion maharusi kuzunguka mabarabarani ili kujionyisha kwa umma baada ya harusi kufungwa.
Mizunguko hii inamaana gani lakini?
Mara nyingi husababisha msongamano wa magari barabarani.
hata kama wakikukera mi nahisi pamoja na kujionyesha huwa kuna neno kwenye sheria ya ndoa kuwa *marriage need to be public* labda wanajifunika ili watu wajue ameolewa au ameoa tena mbaya zaidi ni ile wanapokaa juu ya magari noma kabisa.
Ehe juu ya magari tena! Kama umewaalika watu kwenye harusi yako inamaanisha hao ndiyo uliotaka uwatangazie au wawe ndiyo shuhuda mbele ya mungu! sasa ukipita mitaani ukijidani ndiyo tujueje? Siku ya harusi unatakiwa uwe ndiyo malikia/mfalme ukae uhudumiwe watu wakupongeze pale ulipoandaliwa sio kupita ukizunguka huku na huku (unatafuta nini tena jamani?) Huu ni utumiaji mbaya wa pesa mlizochangiwa kwa mafuta na usumbufu wa wale waliowafuata kusherehekea - Mnawachosha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kay