Harusi ya Messi sasa kufanyika Juni 30, kocha wake wa zamani Luis Enrique hajaalikwa

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Harusi ya mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi sasa ni uhakika itakuwa Juni 30 na itafanyika kwao Rosario, Argentina yeye akifunga ndoa na mzazi mwenzake na mpenzi wake tokea wakiwa shule, Antonella Roccuzzo.

Awali ilielezwa, beki Gerard Pique rafiki wa Messi hakualikwa kwa kuwa mkewe Shakila haelewani na bibi harusi mtarajiwa.

Lakini kinachoonyesha kuwashangaza wengi ni kutoalikwa hata kwa Kocha Luis Enrique ambaye ameamua kuondoka Barcelona lakini madaktari wa Barcelona na kocha mpya, Joaquin Valdes ni kati ya waalikwa.

Sherehe za harusi hiyizo zitafanyika katika hoteli ya Pullman ambayo tayari vyumba 250 vimelipiwa na baadhi ya wageni wamekuwa ni siri.
Pia imeelezwa viongozi wengi wa klabu ya Barcelona hawajaalikwa na Sergio Aguero ni kati ya walioalikwa.

Taarifa nyingine zimeeleza jumla ya watu 21 kutoka katika kikosi cha Barcelona wamelikwa na tayari maandalizi ya โ€œkufa mtuโ€ yameishaanza.

Chanzo: Salehe Jembe
 
Christian Ronardo kaalikwa kweli
 
kama akialika wote wanaofahamiana zitahitajika hotel za mji mzima,wengne wabak nchin kwao wafny kazi..hapa kazi tu
 
Mkuu wamekupa kamwaliko?๐Ÿ™‚๐Ÿ™‚
Kama hakuna mchango naenda sipendagi mie ile michango ya hapa nyumbani Tanzania mtu anakudai utadhani deni, nataka kwenda kula bure tu hahahahahah
 
Ingekuwa bongo ungesikia kuwa Messi kawanyima mwaliko
watu wake wa karibu kwa sababu wao ni CHADEMA.
 
Labda alipewa kadiya mchango akaingia nayo mitini..........Hii hali ya ugum wa kuchangia harusi kumbe haipo kwetu tu
 
Oyo,oyooooo naskia mond ,mzee chibu Platnumz ,yupo nae pia kaalikwa jamani , wapi kiba aah ah chali
 
Huyu andunje kumbe ana roho mbaya kama faru John WA tz!!!!
 
Christian Ronardo kaalikwa kweli
Andunje hawezi kumlipa mnyama cr7, Ronaldo sio wakualikwa tuu, unatakiwa umlipe kabsa!!!

Huyu demu WA andunje Ni mfupi aisee-kistuli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ