Hasani Kesi kachomesha Kaunguza mboga

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Hatumlamu ila baada ya mechi ni wajibu wetu mashabiki kutathimini tumekosea wapi.

Kitendo cha benchi la ufundi kumtoa Salum Kimenya limetughalimu sn. Ni mechi ambayo ilikua upande wetu ila baada tu ya Kimenya kutoka shida ikaanza kutuandama hasa upande wa kulia.Ntatoa sababu

1.Kimenya alikua hapandi mbele kwani yule winga wa kushoto wa Libya ana mbio sn, na ni mbunifu hivyo kufanya Kimenya kukaba vzr na kutompa nafasi kufanya anavyotaka.

2. Kimenya ni mrefu hivyo alisaidia sn kuokoa mipira ya cross.Mfano goli la pili ufupi wa Kesi ulifanya mpira umfikie mshambuliaji alietoa pasi ya goli

3. Kesi alipoingia hakuwa makini hivyo yule mshambuliaji kuwa huru kufanya maamuzi.

4. Magoli yote ukiyaangalia kwa makini makosa ya Kesi yalichangia kwa asilimia 50 mpaka 80.

4. Kwa ujumla upande wa kulia km Taifa ni tatizo japo Kimenya aliweza kuyapunguza.
Bado tuna nafasi kubwa ya kusonga mbele. Tujipange
 
Hilo la kesi moja, pili TFF wasituchanganye kabisa wanazunguka tu kwenye viti maofisini wakisubiri fungu la FIFA wanashindwa kuwachukulia hatua hawa marefa? kama wao hawatoi malalamiko kwa CAF nani ataikomesha hii tabia ya marefa kutuonea
 
Kocha jana sjui aliwaza nn kumtoa Kimenya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…