Hasheem Thabeet: The Tanzanian Phenom

..kuwepo kwa Marc Gasol kwenye team ya memphis ni good news kwa Thabeet.

..hiyo itamsaidia Thabeet kuanza from the bench na kupata muda zaidi wa kujifunza na ku-adopt to the game.

..NBA ni ngumu sana haswa ukizingatia kwamba wanafanya scouting/upelelezi wa hali ya juu kabla ya mchezo.

..kwa mchezaji kama Thabeet ambaye ni mrefu scouts wanaweza kushauri timu pinzani ihakikishe kwamba hapati mpira karibu na basket hivyo kumzuia asi-dunk.

..pia wanaweza kumlazimisha kila anapopata mpira wamuelekeze aende upande ambao hayuko comfortable. hiyo inaweza kumfanya Thabeet awe prone to turnovers.

..kwa msingi huo utaona Thabeet anahitaji muda wa kujifunza moves mbalimbali akizingatia scout reports ili kuweza kuwa mchezaji mzuri ktk NBA.

NB:

..hata Kobe Bryant hakuwa starter ktk mwaka wake wa kwanza NBA
 
Kila la kheri kijana Hasheem,angalia usilewe sifa maana safari bado ni ndefu.
 
Mkuu Joka Kuu, well put..... To our B'ball shinning star, Hasheem go conquer and have the best seasons to come in the NBA!! Go man, its all yours to show what you have in stock for them dudes in the league!
 
Chipukizi Hasheem Thabeetmchezaji kikapu wa Tanzania baada ya kusajiliwa na timu ya NBA ya Memphis Grizzlies anatarajiwa kulipwa USD 14,379.840 sawa na Tshs 19,125,187,200.
Wakuu kumbe kikapu kinalipa zaidi kuliko TFF zetu.kwa nini tanzania huu mchezo usipewe kipaumbele zaidi na hata serikali kuinterven kwa kuoboresha zaidi.?
 
kodi anakatwa bei gani ? za kufanya kazi huko marekani ? , pango la nyumba na mambo mengine hayo unayatoa ? kwa hela hizo ?
 


Umaipata wapi hii??? tupe source plz
 

Ni wazo zuri serikali kuwekeza kwenye michezo hasa Basketball, ila jambo la msingi la kutambua ni kwamba mchezo wa Basketball hasa kimataifa sio kila mtu anaeupenda atacheza, bahati mbaya hautoi fursa sawa kwa watu wenye vimo (urefu) tofauti. Thabeet ana urefu wa ft 7,3 hiyo tu ni credit kwa yeye kuweza kucheza. Swali; Je tuna watanzania wangapi wenye kimo cha Hasheem. Sidhani kama mtu wa kimo cha Mrisho Ngasa hata awe talented vipi kama ataweza kucheza NBA.
 
Chaku, usiamini haraka kila unachokikuta kwenye mtandao.
CNBC.com wana article moja tu inayomtaja Hasheem Thabeet ukitumia search.
Halafu mwandishi mwenyewe (wa Mwananchi) hajui kuandika.


 
Chaku, usiamini haraka kila unachokikuta kwenye mtandao.
CNBC.com wana article moja tu inayomtaja Hasheem Thabeet ukitumia search.
Halafu mwandishi mwenyewe (wa Mwananchi) hajui kuandika.
Bwaha ha ha ha ha mkuu magazeti ya bongo utafikiri yanaandikwa na wahariri wa Milembe
 
Last edited:

Kikapu kimewalipa wangapi?
Ligi ngapi za Kikapu zinalipwa vizuri?
Demand ya wachezaji wa KIKAPU na TFF ipi kubwa????
Mchezo gani unawaburudisha wa TZ wengi kati ya KIKAPU na TFF?
?????
??????
?????????
Alafu niliwashangaa sana watangazaji wa CLOUDS FM, eti watanzania hawajui HESHIMA aliyopata huyu dogo na hawajui ni kwa kiasi gani NBA iko juu jamani jamani.........
 

Somebody needs a math coach, and to get a life.

Now I understand kwa nini yule mchizi aliyeenda kupiga boli Norway hakutaka mshiko wake utajwe, wabongo hawakawii...
 
Hiyo figure sidhani kama ni sahihi. Nadhani atakuwa anachukua kama $4 mil kwa mwaka. Plus hela za kutangaza bidhaa, ambazo ndo zinakuaga nyingi. Kama sikosei Shaq anachukua mil 20, so rookie kuchukua 14 itakuwa hatari.
 
I think that figure is over three years not one year.
 
Yule nae anaweweseka...tu dunia nzima mikataba inatajwa sembuse yeye....hashiem amepania kununua mtaa wao sinza.....twamngojea.hy pesa aje awekeze kwao aongeze mzunguko.....
 
Hebu gonga katika link hii hapa (((HOOPSWORLD))) utaona mishahara ya Memphis Grizzlies ilivyo. Hapa bado jina la Hasheem halipo, ni kwa wale waliopo. Je Thabeet anaweza wapiku hawa wakongwe?? HOOPSWORLD
 
Sio rahisi kuiweka BILIONI kwenye uwiano ukaelewa billioni 19 ni fungu la namna gani.
Ikiwa aliyesema mabilioni yaliyochotwa BOT (130 bil.) yana uzito wa tani 50 yuko sahihi, basi billioni 19 zitakuwa na uzito wa lorry kubwa la tani saba! Now, picture that some of money in your bank account 🙂
 
Chipukizi Hasheem Thabeetmchezaji kikapu wa Tanzania baada ya kusajiliwa na timu ya NBA ya Memphis Grizzlies anatarajiwa kulipwa USD 14,379.840 sawa na Tshs 19,125,187,200.

Guyz, according to mtandao wa cnbc, huu ni mkataba wa miaka mitatu, kwa hiyo hiyo pesa ni malipo ya miaka mitatu. Ni ndefu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…