Pre GE2025 Hashim Rungwe ashinda uenyekiti CHAUMMA kwa mara ya tatu, aahidi kushikilia sera yake ya ubwabwa mashuleni kwenye uchaguzi 2025

Pre GE2025 Hashim Rungwe ashinda uenyekiti CHAUMMA kwa mara ya tatu, aahidi kushikilia sera yake ya ubwabwa mashuleni kwenye uchaguzi 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashimu Rungwe, kwa mara nyingine ameibuka kidedea baada ya kutetea kiti chake kwa ushindi wa kura 118 kati ya 120 katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Mohamed Masoud, alieleza kuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti alikuwa mmoja tu, ambapo wapiga kura walichagua kwa njia ya ndiyo au hapana.

Rungwe alifanikiwa kupata idhini kubwa ya wajumbe kwa muhula wake wa tatu tangu chama hicho kianzishwe.

Baada ya ushindi wake, Rungwe aliwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kuendelea kumuamini, huku akiahidi kuendelea kusimamia sera yake maarufu ya Ubwabwa mashuleni na hospitalini.

Pia alisisitiza kuwa mpango wa chama cha CHAUMMA kupeleka bahari Dodoma uko imara na utaendelea kusukumwa mbele.

Source: Kuelekea 2025 Mazungumzo ya Upinzani kusimamisha mgombea Urais wa pamoja 2025 yanukia

Naibu Msajili kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Sist Nyahoza, alikipongeza chama hicho kwa kufanya siasa kwa njia ya amani na kufuata misingi ya kitaifa kama vile utulivu na mshikamano.

Source: EATV
 
Back
Top Bottom