Hasira

Hasira

Bebz

Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
80
Reaction score
12
Habari,
Natumai wazima uku. nina tatizo sasa sijui ni ugonjwa au vipi na kama si ugonjwa ningependa ushauri kutoka kwenu.

Nahitaji msaada wenu kwani nimekua mtu wa hasira/ short tempered na hasira zangu si zile za kupiga/kuumiza mtu au vipi lakini kuongea sana na pia imekua ikinitokea karibu kila mwezi mara moja na mara nyingi kwa mtu alie karibu yangu,mpenzi au rafiki na pia inanipelekea kuwa na maamuzi ya haraka sana na baada ya masaa huwa najirudi na kujuta na kujiuliza kwa nini nifanya/kusema vile.
Saa nyingine huwa naamua nakaa mbali na marafiki au kuepuka kudate mtu maana naona ntamuumiza hisia zake na inaniogopesha kwani naweza kukosa mtu wa kuishi nae.

Naombeni ushauri/msaada wenu.
 
Bila shaka wewe ni binti, na sio wewe anaefanya uwe na hasira, huyo ni roho unatakiwa upate huduma ya sala na toba kwa watumish wa Mungu(genuine kama Rev Lawrence Magike) wa kiseke Mwanza.

Usihofu in an eye-blink u will be set free
 
Asante lakini nimeshafanya sala ya toba,hata sijui sasa nichukue hatua gani tena.
 
Jaribu hili,kunywa maji ya moto/uvuguvugu kila unapojihisi hasira zimepanda,fanya hivyo kwa wiki mbili then unipe feedback ili nikupe ushauri mwingine kama huo haukufaa!
 
Jaribu hili,kunywa maji ya moto/uvuguvugu kila unapojihisi hasira zimepanda,fanya hivyo kwa wiki mbili then unipe feedback ili nikupe ushauri mwingine kama huo haukufaa!
asante acha nijaribu hiyo
 
Bebz,

Pole, mara nyingi matatizo kama haya husababishwa na chanzo/kiini...mfano, msongo wa mawazo kupoteza kitu/mtu, matatizo kazini/familia n.k.. lakini haimaanishi kuwa watu wote wana vyanzo hivyo.

Kupitia kujua kiini/chanzo ni njia rahisi, pili kutamvua kuwa ni tatizo na linahitaji ufumbuzi husaidia sana katika kupata tiba.
Zipo njia kadha wa kadha mfano ku_control pumzi/upumuaji wakati wa hasira, kutumia maji n.k zimeweza kusaidia watu.

Ni vyema kuonana na mshauri wa Saikolojia mahali ulipo, au katika hospitali kutafuta kitengo cha magonjwa ya akili kwa msaada zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Joto hasira ambaa tiba tafuta mtu awe anakufikisha kileleni tatizo lako litaisha.
Copy: Yahya aka Ruge
 
Last edited by a moderator:
Joto hasira ambaa tiba tafuta mtu awe anakufikisha kileleni tatizo lako litaisha.
Copy: Yahya aka Ruge
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom