Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Aliyekuwa Mbunge kwa tiketi ya CCM (2010 - 2015) Hasnain Murji awahimiza wananchi Mtwara kushiriki kwa kujiandikisha katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Hasnain aliyasema hayo mara baada ya kujiandikisha Oktoba 18, 2024 katika mtaa wa Shangani West, ambapo aliwasihi wananchi na hasa wanachama wa CCM kuhakikisha wanajiandikisha, akisema ni vizuri kila mwenye vigezo ajiandikishe ili apate fursa ya kumchagua kiongozi ambaye ataleta maendeleo kwenye maeneo husika.
Kupata taarifa za mikoa yote uchaguzi serikali za mitaa soma: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Huku, mjumbe wa Halmashauri kuu CCM mkoani humo bwana Mohammed Abdallah Mohammed amesema wameamua kuungana na kuhamasisha wanachama ili wananchi waweze kujitokeza kwenye zoezi hilo na wapate viongozi wanaohitajika katika jamii na watakaoleta maendeleo.
Pia soma:
LGE2024 - News Alert: - Dodoma: Rais Samia ashiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Mtwara Digital