Hassan Kessy ruksa kuichezea Yanga

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Baada ya kelele kadhaa NA dhihaka zisizo NA msingii kamati ya sheria NA hadhi ya wachezaji imeidhinisha rasmi mchana jina la HASSAN KESSY KUICHEZEA YANGA BILA MASHARTI YOOYOTE
 
Baada ya kelele kadhaa NA dhihaka zisizo NA msingii kamati ya sheria NA hadhi ya wachezaji imeidhinisha rasmi mchana jina la HASSAN KESSY KUICHEZEA YANGA BILA MASHARTI YOOYOTE
Mkuu, sio bila masharti yoyote. Hukumu ni kwamba anaruhusiwa kuichezea Yanga muda wowote kuanzia sasa lakini baada ya kuilipa Simba sh. milioni mia mbili (200M) kama fidia ya kuvunja mkataba. Kumbuka Kessy alianza kuitumikia Yanga kabla hajamaliza mkataba uliokuwa unaisha Juni 17

 
sasa mbona juzi walimrusu akacheza mechi ya yanga.? au alisha lipa?
 
Bakini NA mashartihewa
 


Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji imelipitisha jina la mlinzi wa kulia wa Yanga Hassan Kessy Ramadhani kuitumikia klabu hiyo baada ya hapo awali kuwepo na mvutano mkubwa na klabu yake ya zamani Simba SC.

Simba ilikuwa ikimtuhumu Kessy kuvunja mkataba kwa kuanza kuvaa jezi, kufanya mazoezi, kusafiri na kushiriki shughuli mbalimbali za mabingwa hao wa VPL msimu uliopita wakati muda wa mkataba wake na Wekundu hao wa Msimbazi haujafika kikomo.

Kutokana mgogoro huo, klabu ya Simba haikutoa barua (release letter) kumruhusu Kessy kuitumikia Yanga ikidai kulipwa fidia na mchezaji huyo kwa kuvunja mkataba. Sakata hilo lilimfanya Kessy kushindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga katika michuano ya kimataifa licha ya kuendelea kufanya mazoezi na kikosi cha Hans van Pluijm.

Uamuzi huo unamfanya Van Pluijm kuwa huru kumtumia Kessy kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara kuanznia msimu mpya wa 2016/17 pamoja na ile michuano ya kimataifa ambayo Yanga wataiwakilisha Tanzania kwenye klabu bingwa Afrika.

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji awali ilikuwa ikutane Jumanne lakini ilishindikana na baadae zikatoka taarifa kwamba, wachezaji wote walioombewa leseni na vilabu vyao wataruhusiwa kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Jumatano kati ya Yanga na Azam huku Kessy aliitumikia Yanga.

Leo Ijumaa August 19 taarifa zimetoka kwamba Kessy yuko huru kuitumikia Yanga baada ya kamati hiyo kukaa na kupitia kesi zote za usajili ikiwemo ya Kessy.
 
Afadhali kijana wa watu apumue Yanga na Simba ubabaishaji mwingi,mambo yapo Azam
 
Simba sasa wapeleke madai yao Yanga. Yatafikiriwa lakini haitazuia Kessy kuichezea Yanga.
 
Simba sasa wapeleke madai yao Yanga. Yatafikiriwa lakini haitazuia Kessy kuichezea Yanga.
1.Kessy alikuwa anaitwa mamluki alivyokuwa Simba (Viongozi ndio walisababisha wanachama/wapenzi nao wakaamini) Wakaanza kumzomea na kumtukana


1.Simba hawakumtaka Kessy ndio maana waligoma kumuongezea mkataba mapema baada ya yeye kudai madai ya mkataba uliokuwa unaisha

2.Baada ya mechi ya Toto Simba walimfungia Kessy mechi 5 na asingecheza tena hadi msimu unaisha na mkataba wake ungeisha

3.Kessy kusafiri na timu sio kigezo kuwa amesajiliwa/kusaini mkataba

4.Sijui Hans Pope atajifunza lini issue ya Twite, Yondani, Ngasa, Singano, Tambwe, Maguri, Kiiza zote amechemsha
 
Hans Poppe anawepelekesha sana Simba. Cha ajabu ni mtu was kuteuliwa tu kwenye kamati lakini sauti kuliko aliyemteua
 
Huyu jamaa sijui tatizo ni elimu, au huwa anajitoa ufahamu makusudi ??
 
Unatakiwa utambue kuwa Simba SC ilishindwa kumlipa Kessy mshahara wa miezi mitatu. Mkataba unasema kama klabu ikishindwa kutii vipengele vya masilahi ya mchezaji, basi mkataba unakuwa umevunjwa.
 
Duh!
 
Sasa izo pesa analipa kessy au yanga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…