Hata angekuwa hai alikuwa na kinga ya kutoshtakiwa, tumuache apumzike. Ndoa ya Kikristo ikishafungwa haina zuio tena

Hata angekuwa hai alikuwa na kinga ya kutoshtakiwa, tumuache apumzike. Ndoa ya Kikristo ikishafungwa haina zuio tena

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwa mujibu wa Katiba ya JMT Rais ana kinga ya kutoshtakiwa.

Ndio sababu tuna Bunge ambalo linaweza kumshughulikia pindi anaposhindwa kutekeleza Majukumu yake ipasavyo.

Sasa kama Bunge lilishindwa kushughulika na hayati Magufuli akiwa madarakani hilo ni tatizo la Wabunge siyo JPM.

Kwenye Ndoa ya Kikristo kasisi husema "Mtu yoyote mwenye Zuio la Haki Watu hawa wawili wasiungane kwenye Ndoa Takatifu na aseme SASA au anyamaze MILELE."

Hii ni Sawa kabisa na Rais wa JMT ukishamkosa awapo madarakani ndio imetoka hiyo yanayobaki ni kama mayowe ya Ufipa St. huwezi kumshtaki popote kwa mujibu wa Katiba, Wabunge Mungu anawaona mjue.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Kinga za kutoshitakiwa zifutwe na wote waliotenda, wanaotenda maovu kwa kisingizio cha kinga ya kutoshitakiwa, tuwashitaki na waadhibiwe pindi ilithibitika wana hatia🤔
 
Lazima yasemwe na kuandikwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kwanza aje achue hatuvihitaji (vyakuokota) mama kaagiza vpya.

DDA.jpg
 
Yesu Kristo anasemwa kwa yote aliyofanya kipindi alichokuwa hapa dunia kimwili.
Mohamed anasemwa kwa yote aliyofanya alipokuwa hai duniani.
Hitler na Musolini wanasemwa kwa uovu waliofanya wakiwa hai!
Nyerere, Nkurumah na Mandela nao wako midomoni kwa watu hadi leo.
Addi amini na Mobutu hivyo hivyo kwa unyama wao.
Sasa magufuli ni nani hadi asisemwe? acha asemwe kama wengine wanavyosemwa kwa ubaya au uzuri!
 
Katiba inatoa kinga kwa mtu aliyetenda kwa mujibu wa madaraka ya urais na siyo akiwa rais.

Katiba inampa rais madaraka kadhaa, na aakifanya kosa katika harakati za kutekeleza wajibu wa kikatiba ndipo anakuwa na kinga ila akitenda kosa katika harakati zaa kufanya yaliyokinyume na matakwa ya katiba hapo hana kinga.

Mfano, katiba haisemi kwamba rais ana madaraka ya kuua na kutesa watu. Sasa akitenda makosa haya, hapa hana kinga. Acheni kudanganyana!
 
Back
Top Bottom