Hata baada ya kujua Mgombea wa CCM ni Magufuli, why kuna watu bado wanaleta mizaha? Kunashusha hadhi ya Urais wetu!

Mkuu Paskali, ulishawahi kutukumbusha hapa jukwaani kuwa demokrasia ina gharama zake. Kwa hiyo pamoja kutegemea CCM kuishi kwa mazoea ya utamaduni iliyouzoea, lkn sasa imejitokeza gharama ya kutekeleza matakwa ya katiba ili "the incumbent" akapate kushindanishwa na watia nia wengine.

Kuna haja pia chama kuingia gharama za ziada kuchapisha fomu za hao watia nia wengine, wala isibakie ile moja tu iliyokwisha kutolewa. Ebu jaribu kufikiria endapo mtia nia mwingine angaliwahi kuzichukua fomu hizo, hivi kweli ingeingia akili kumwambia Mwenyekiti kuwa akachukue nakala kwa yule aliyemtangulia?
 
Pascal Mayalla,
Imenifurahisha kauli yako ya 'call a spade a spade' kwa kuwaainisha wanaotaka kupambana na JPM kwenye uchaguzi ujao kuwa 'wanafanya mzaha', sawa na kupambanisha Heavy Weight (wa hadhi ya Mohammed Alli au Mike Tyson) na bingwa wa Tanzania. Matokeo ya pambano kama hilo ni dhahiri.

Hata hivyo, kwa vyama vya upinzani, ruksa kutumia haki yao ya kikatiba kusimamisha mgombea. Wiki jana msemaji wa Baraza la Wazee wa CHADEMA, alipokuwa akizungumzia kushambuliwa na kuvunjwa mguu kwa Mbowe, alisema kwamba watashinda Urais, viti vyote vya ubunge na udiwani nchi nzima kwa asilimia 100!

Kauli kama hiyo kweli tunaweza kusema ni 'mzaha' wa kustarehesha baraza. Pamoja na kwamba watu waruhusiwe kutumia haki yao ya kikatiba, muhimu ni kwamba kusiwe na maneno neno yasiyo na tija baada ya uchaguzi. Anayejisikia kutoridhika na matokeo, apeleke dukuduku yake mahakamani kwa heshima tu na uamuzi wa mahakama uwe ndiyo mwisho. Tukifanya hivyo, itakuwa ndiyo demokrasia yenyewe, hata kama Paskali atakuja kusema 'Si niliwaambia?'
 
Hayo ni maoni yako, ila ni bahati mbaya umewavunjia wengine heshima. Akitia nia ya uraisi mtu wa tabia isiyefaa, mwache, ni haki yake ya kikatiba. Hakuna mzaha hapo:
Mtu wa ajabu na mwenye mzaha ni yule atakayempa kura mgombea asiyefaa.
 
Pascal Mayalla uwepo mdahalo wa kuwakutanisha wagombea wa kiti cha urais wa vyama vyote ndiyo tupime hiyo mizaha uliyobaini
 
Halafu Pascal, kutaja kuwepo mdahalo wa kitaifa hujui ni kauli hatarishi kwa maisha yako?
Anyway, nilikuwa naku tahadharisha tuu na kauli hiyo kwani kuna watu wana nguvu sana hawaipendi hiyo kauli kabisa
 
Kujikomba kumekulipa sasa press card yako imerudishwa baada ya kuona unataka kuwa kichaa sasa kwa kusifu na kuabudu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…