Hata baada ya kujua Mgombea wa CCM ni Magufuli, why kuna watu bado wanaleta mizaha? Kunashusha hadhi ya Urais wetu!

Makala yako hii inaonyesha una mashaka na mgombea wako kwamba akitokea mtu wa kuaminika utakosa maslahi ikiwa upande wk yupo mmoja una lalamikia nini upande wa pili?
Na kama unamuona ww huyo wa kwako anafaa wape ruhusa na wangine wapendekeze wa kwao wanaowaona wao anafaa usiamue kwa akili yako peke yako
 
Kuhusu Urais JPM kashamaliza na bila shaka atapita kwa kura nyingi kuliko 2015.

Dar kulikuwa eneo gumu sana kwa CCM 2015, maana alizomewa sana wakati anapita kugombea.
Muda ni mwalimu mzuri, juzi kapita ubungo na kuketi huku watu walewale waliomzomea walikuwa wakimshangilia.

Kwa muktadha huu, JPM ameweza ku-turn around the wheel.

Ushauri wangu mwaka huu baada ya uchaguzi,
Wizara za Kilimo, mifugo na Uvuvi, wizara ya vijan na ajira, wizara ya viwanda asifanye uteuzi wa moja kwa moja.
Atafute watu kwa head hunting wenye capacity ya kugeuza mazao ya kilimo kuwa asset ya kuchakatwa na kuuzwa nje ya Tanzania kama consumable products.
In the course lazima tafsiri ya kinachofanyika,
Kiongeze ajira, tax base, forex na kupunguza imports.

Imetosha ku-import sukari wakati ardhi ipo, maji ya kumwagilia yapo na soko la sukari lipo kwa consumable sugar kwa matumizi ya binadamu na kwa matumizi ya viwanda.

Itoshe mpaka ku-import chupi wakati tuna pamba Tanzania.

Akifanya haya JPM will make it to be the best president to happen in our generation.

Watanzania wenye know how to see the industrial economy is becoming real tupo.
We just need to a financial leverage to be set ili kupatikana kwa technology na consultants wa kutu-guide namna ya kuzalisha products zinakokidhi ISO certifications.

Shalom.
 
Nionacho kaka/baba yangu Pasco unaendeleza kosa lile lile la kulaumu matokeo bila kujitafakari tumefikaje hapa. Hebu angalia hata watia nia wa ubunge, angalia hadhi ya ubunge ilivyo sasa na miaka ya nyuma kama ipo sawa.

Kuna makosa makubwa tumeyafanya, makosa hayo (Sitoyaeleza hapa ili kutoa fursa ya tafakari pana) ndio yamepelekea kuona kumbe mtu yeyote anaweza kupewa dhamana kubwa ya kiuongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa.

Kama taifa tusipofanya tafakari ya kitaifa na kurudi kwenye misingi bora, tutajikuta tunapata viongozi vituko vya ajabu huko mbele.
 
Why mnatumia nguvu nyingi sana kumuuza mtu mnaedai kafanya makubwa???
Acheni kupiga mayowe...waacheni wananchi wayaone wenyewe.
 
Yeye wakati anagombea walikuwa wagombea 42, na hakuna aliyebezwa, ingawa tuliona walimrahisishia njia kwa kumfukuza Lowassa uanachama, lakini narudia walikuwa wagombea 42. Alipitishwa kimizengwe na kutangazwa kimizengwe.

Lakini wale wote waliogombea naye bado wengi ana bifu nao na hataki hata kuwaona licha ta kuwasikia.

Wapo waliopenda kujipima tena, lakini yeye mwenyeketi hataki kuruhusu wenzake wapate kujipima kuchaguliwa.

Kesha jichagua na hataki wengine eti yeye pekee tu.

AJITANGAZE BASI KWAMBA YEYE NDIYE RAIS.

Kwanini hata nje ya ccm hataki kuwe na wagombea?!

Mambo ya kujidai unajua wewe tu kila kitu, eti bila wewe haiwezekani huo ni ujuha.

Zanzibar waachwe watafute mgombea kwa utaratibu wao na wasiingiliwe.
 
Kipimo cha uhovyo wa mtu unao wewe? Sifa zote za hovyo hovyo ulizoainisha mbona JPM anazo???!!!
Uzinzi yeye, utekaji na mauaji yeye (kashindwa kuzuia), kubeep urais na ujinga mwingine kibao. Hao wengine ni afadhali kuliko jamaa yako!
 
Raisi JPM aachwe amalize muda wake wa miaka 10

Baada ya hapo ipo jikoni raisi mwingine wa aina ya JPM aja kwa 2025-2030, 2030-2035

Ni katika ileile kuondoa mizaha kwenye taasisi ya uraisi.

Kuna watu wengi wanasifu yalotokea Malawi lakini wanasahu kuwa chama cha DPP tangu kiingie madarakani miaka 26 ilopita kimeleta mizaha na hakuna kilichofanya.

Polisi wa Malawi wanaongoza kwa kupokea rushwa na wafanya biashara wadogo hawana uwezo wa kushindana na wale wafanyabiashara wageni hivyo kufanya miasha yao kuwa magumu kiuchumi.

Makamu wa raisi Mutharika bwana Chilima alikuwa akimwangalia tu raisi huyo alieendekeza mizaha na kujisahau, huku kimyakimya akiwaandaa MCP na Dr Chakwera kurudi madarakani baada ya miaka 26.

Pili, watu wanasahau Malawi iliongozwa na serikali ya mseto huku Chilima na wenzake wakijiandaa kukusanya kura kwa wingi kutoka majimbo ya chama cha DPP na hivyo kufanya ushindi wa safari hii kuwa wenye nguvu.

Sasa Tanzania haina serikali ya mseto na haihitaji kuwa nayo kutokana na upande wa upinzani kuwa uko likizo na umelala usingizi na unakusaya ruzuku kila mwaka.

Pili, wapinzani wamekuwa wanaleta mizaha tangu siasa za vyama vigi vianzishwe mwaka 1992 maana wangefanya hivyo, basi mwaka 2015 wangemsimamisha Dr Slaa badala ya kubadili gia angani na kwa kumleta Edward Lowasa ambae alitoka CCM.

Nafahamu watasema wamekuwa wakionewa wakati hawana mbinu mbadala za kutengeneza mikakati ya namna ya kukabiliana na CCM, na badaa yake wamekuwa wakikosea kila eneo la mikakati yao hivyo kujikuta wakikumbana na polisi na vyombo vya dola.

Hatuna mizaha kwenye maslahi, mstakabali na "future" ya kizazi chetu cha baadae.
 
Hii kuluhusiwa kuchukua form kwa watu wengi, ni mbinu ya shambulio la kushtukiza.
Adui asijue na hasa anaetakiwa kupewa urais.


Kama unakumbuka 2015 wangeluhusiwa wachache kuchukua form,basi ingekua lahisi wahusika kuumizana.

Na hata 2025 wataluhusiwa wachukue form wengi tu.ili.wale.wenye vibuli kwa sababu ya umaalufu wao waangushwe vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…