Hata baada ya kujua Mgombea wa CCM ni Magufuli, why kuna watu bado wanaleta mizaha? Kunashusha hadhi ya Urais wetu!

Nimeguswa uliposema Wauaji wamechukua form
Kwanza turudi nyuma,Nani alimpiga Lissu Risasi ?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Yaani maoni yoooote hayo na maswali hukupata hata udc?,
 

Duh, Pascal wewe ndio unaleta mizaha. Hizo sifa hasi ulizotaja ndizo zao wanasiasa wa mikakati. Jihadhari tu usijeeleweka vibaya na usiowakusudia! Bila shaka pia ulishawahi kusikia mjadala wa paradox ya mtu aliyesifiwa kuwa “a honest politician” - maneno mawili yasiyoweza kamwe kuwa kwenye sentensi moja. Sasa unayemuona mwanasiasa makini lazima awe na hizo sifa maalum.
 
Makala ndefu yote hii ya nini,wakati hata ambaye tulie naye sasa hivi mwenyewe alikiri kwa kinywa chake kuwa alikua anajaribu(ndio masulihala yenyewe haya) then akasukumizwa.
Mayalla Bado anatafuta uteuzi wa JIWE hivyo msishangae na makala zake kuwa ndefu; he is on a publicity stunt!! Mayalla ana njaa.
 
Umesahau Kuna wadanganyifu wa uraia pia......Kuna hadi wanyarwanda wanagombea nafasi za juu kabisa za ukuu....au kwako hao ni watakatifu
 
Acha kujikomba komba! Huoni aibu kujikomba komba kila kukicha ili kutafuta teuzi? Tangu lini fisadi na dikteta anastahili kuwa na HADHI?

Hadhi ya mtu haitolewi kama njugu kutokana na cheo chake bali ni kwa matendo yake MEMA
 
Makala ndefu yote hii ya nini,wakati hata ambaye tulie naye sasa hivi mwenyewe alikiri kwa kinywa chake kuwa alikua anajaribu(ndio masulihala yenyewe haya) then akasukumizwa.
Mkuu Kateli, ni kweli rais Magufuli hakujua kuwa yeye ndie angekuja kuwa rais wetu, na pia ni kweli yeye anajihesabu alikuwa anajaribu tuu kwa ku beepu tuu mara ghafla simu ikapokelewa.

Soma tarehe ya bandiko hili
Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Jee umepata kitu?.
Na kwa faida ya wale walio busy hawana muda wa kufungua link,
P
 
Twende Sawa Sawa Na
John Pombe Joseph Magufuli
Atatuvusha Ila Sasa Akituacha Oops!!
Tumchague Nani Tena Ccm
🤨😑😶😎
 
Yesu alionya Mafarisayo na Waandishi kwa kuwaita "WANAFIKI"
MAFARISAYO NA MASADUKAYO! Ndio waandishi wa kizazi hiki, kuna mengi ya kuhoji ila anaona yatamkosesha teuzi, ila tatizo aliingia na mguu wa kushoto katika awamu hii kwa lile swali lake la siku ileee
 
Wao ndio wana mizaha, kujengeana nyumba kama vile hawana huku wakijigamba lazima wajengewe kutokana na sheria! As if wanalala nje?! Wakati kila raia anajuwa wanayo mahekalu ya kutosha, wakisahau raia bado wana shida ya maji, miundo mbinu na malazi..
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…