Hata ikisainiwa kwa mbwembwe; sheria hii bado ni mbaya!

Sheria inaweza kuwepo lakini je itafuatwa?
Kwani kipindi kile Jakaya Kikwete huyu anahonga watu ili aingie Ikulu sheria zetu hazikuwepo? ......alichokifanya kununua Uraisi kilikuwa sawa kisheria?
 
-Hii sheria inawasaidia sana hasa vijana wanaogombea

-Pia hebu tuone jinsi ambavyo inaweza kuvunjww

.kutumia watu/wachangiaji bandia

.Pia je nikitoa hela halafu nikawapa watu wakaitana kwenye hafla,tafrija halafu wakanikaribisha na nikapewa fursa ya kuwahutubia.Sheria hii itakua imenibana,coz mimi ndo nitakua nimekaribishwa lakini ukweli ni kwamba mimi ndo nimetoa na hafla,tafrija au chakula na vinywaji vitakua vimeji-associate na jina langu

.Je nikigawa hela kwa vikundi mbali mbali vikanipigia kampeni halafu wakatumia lugha kwamba wamejitolea bila malipo kunipigia kampeni itakuaje?

Nitarudi tena hapa kuchangia tuone jinsi sheria hii inavyoweza kuvunjwa!
 
Mwanakijiji,
Obvious utakuwa unayo kopi ya huo waraka wa sheria. Je unaweza kutusaidia kuu-attach kwenye hii post ili tuukague kama tutakuwa na muda? Thanks in advance.


sheria ipo kwenye ile mada ya expenses
 
By GABRIEL NDERUMAKI (Daily News),

IT was a historic moment in the country's politics today when President Jakaya Kikwete assented the Election Expenses Bill into law at a brief but colourful ceremony at State House in Dar es Salaam.

The well attended function which was also beamed live on a number of local TV stations, marks the start of the new law whose bill passed through a bumpy process in the parliament before it was finally endorsed on February 11, this year.

This was also the first time ever in the country's history the head of state had signed a bill into law before the public.

The new law aims at creating a proper and more conducive mechanism for governing of campaigns and election financing, seeks to make provisions for funding of nomination process, election campaigns and elections with a view to control the use of "dirty" funds.

It also prevents illegal practices in the nomination process, election campaigns and elections. Further, it seeks to provide for the allocation, management and accountability of funds used in campaigns and elections.

In his introductory remarks before the president had signed the bill, the Minister of State in the Prime Minister's Office (Policy, Co-ordination and Parliamentary Affairs), Mr Philip Marmo, highlighted specific areas covered by the new law. They are bribery, treating (takrima), undue influence, Impersonation, corrupt inducement of withdrawal, interference with a lawful public meeting, defacement of notices, false publication of withdrawal, furnishing false evidence and making of false statements.

He mentioned other areas banned under the new law as public meetings and display of emblems in vicinity of polling stations on election day, disclosure of secrets at elections, offences relating to nomination papers or ballot papers, offences relating to registers and certificate of registration.

Others include unfair conducts during the nomination campaign or election, failure to disclose funds, unconscionable funding and finally the conveyance of voters.

"The enactment of the new law was necessitated by the fact that there have been complaints from different quarters in the recent times that there was no level playing field for all contestants", he said.

As a result, he said, wealthy contenders and political parties seized the opportunity to spend freely and make the race a one-sided show.

"This is not a good trend in a democratic state especially on councillors, Members of Parliament and even the President to depend entirely on money to be elected into a public office," he said.

However, he admitted that it was impossible to have a complete ban on financial spending during elections.

"But, this is a new law to start with, let's all support this move which shows the sincere resolve by the government to fight corruption during elections," he added.

The Registrar of Political Parties, Mr John Tendwa, said that all preparations for the new law to be implemented have been done.

"This is a good law that has addressed all weaknesses though it's the first time we have this kind of legislation," he said, adding: "In fact, Tanzania has become the first country in SADC (Southern African Development Community) to have this law".

He said the law would apply in the coming general elections in October on both Tanzania Mainland and Zanzibar. He said that, new zonal offices in Arusha, Mwanza and Mbeya would be operational by April 15.

Mr Tendwa said that his office has drawn up regulations that would be discussed during a two-day joint meeting with all stakeholders which starts on March 22. He said that his office will work closely with other stakeholders like the Adult Education Institute and the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) which have a nationwide network to raise public awareness about the new law.

Chairman of the opposition Civic United Front (CUF), Prof Ibrahim Lipumba who also attended the function said that the new law has given ‘too much' powers to the political parties registrar.

"We also need to look at the powers that have been vested on the political parties registrar. There needs to be checks and balances," he said.

"The registrar lacks internal capacity to make this law work effectively", he said.

National Chairman of the Tanzania Labour Party (TLP), Mr Augustine Mrema, was upbeat about the new law, saying it's a saviour to ‘people like him' who have no big money to spend at will.

"The new law will take all of us, even the poor, to paradise", he said.

The function was also attended by the Prime Minister, Mr Mizengo Pinda, diplomats and Chairman of the National Electoral Commission (NEC), Judge Lewis Makame.
 
Hizo mbwembwe tushazizoea manake ni mzee wa misifa na pomps kibao. Kwa huu upungufu ndani ya sheria sidhani kama inatufaa sisi watz!
 
Naomba nifahamisheni sheria hii itatumika upande wa Zanzibar katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar na wajumbe wa Baraza La Wawakilishi?


hapana.. itahusu wabunge jamhuri ya muungano wa Zanzibar..
 
JK asaini sheria ya matumizi ya fedha kwenye uchaguzi leo

JK akisaini sheria ya matumizi ya Fedha Kwenye Uchaguzi katika viwanja vya ikulu jijini Dar leo huku viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini wakishuhudia
From Michuzi blog
 
Hii picha itarudi kuwaumbua mashahidi waliosimama kupitisha utawala wa kiimla wa chama kimoja. Mtakuwa mashahidi wangu kuwa wengine tumeipinga on the get go!
 
Sheria za kuzuia mambo kama haya zilikuwepo tangu zamani. Sheria ya kuzuia rushwa ilizuia matumizi ya fedha kuwahonga wapiga kura lakini bunge likaibadilisha na kuiita takrima.
Mahakama ilitamka wazi kuwa takrima ni rushwa lakini hakuna aliyechukua hatua zaidi.Hii ilimaanisha kuwa serikali iliyoko madarakani iliingia kwa kutumia rushwa (takrima)
Utiaji sahihi wa sheria hii kwa mbwembwe nk unaashiria kuwa tuna tatizo kubwa la rushwa katika uchaguzi; inadhibitisha kuwa serikali iliyoko iliingia kwa rushwa.
Swali langu hapa ni kuwa -serikali iliyoingia madarakani kwa rushwa, ina uhalali gani wa kuongoza? Je maamuzi yake mengi si yatakuwa ya kirushwa rushwa tu? Haya ndiyo tumeyaona katika awamu ya JK - kulindana.
Hii sheria mpya haitafanya kazi kwani sioni nani katika takukuru anaweza kumkamata mgombea urais wa ccm eti katoa rushwa! Kama zilivyo sheria nyingi, hii itawakamata vidagaa tu. Ebu angalia CCM walichofanya: wamehakikisha wanapokea misaada toka nje halafu ndipo wanapitisha sheria (si mlimuona Msekwa ?); wagombea wao watarajiwa tayari wameshapita ta kuchinja ng'ombe, kuhonga pesa - halafu eti sheria ndipo inasainiwa!
Takukuru ilipaswa kutumia hukumu ya mahakama kuwa takrima ni rushwa kuwakamata - lakini mmhhh...
 
hivi walipopitisha sheria ya TAKUKURU ya 2007 kwanini hawakufanya mabadiliko kuhusu rushwa katika uchaguzi? makosa ambayo wanayataja leo kwanini hawakuyaingiza kwenye sheria ya TAKUKURU.. au rushwa ya uchaguzi ni rushwa nyingine tofauti na rushwa za kawaida?

Hamna lolote.. kushabikia sheria hii ni sawa na watu walioshabikia Sheria ya Madini ya 1998 (ambayo hadi leo wameshindwa kuibadilisha!), ni sawa na kukumbatia sheria ya maadili ya viongozi ya 1998 (ambayo wameshindwa kuibadilisha); ni sawa na kushangilia sheria ya usalama wa taifa ya 1996 (ambayo bado ni sheria mbovu kabisa na wao wanajua hili na hawajaibadilisha).. ni sawa na kushangilia sheria ya fedha ya 2001 na mabadiliko yake ya 2004

tunaambiwa ati mbona kunasheria nyingine mbaya ambazo hatukuzilalamikia; yaani kwa vile kuna sheria mbaya kama hizo hapo juu basi Watanzania tufungue makanwa yetu na kupokea sheria nyingine mbovu kama makinda ya ndege yanavyopokea minyoo! Tusihoji kwa vile hatukuhoji huko nyuma (wengine labda hawakuhoji!)..

Ni fikra potofu kukumbatia uongo leo kwa sababu tuliukubali uongo mwingine huko nyuma.
 
Kwanza,hii bill haikusainiwa kwa mbwembwe. Rais alionekana kama vile anaona haya kuweka saini kwenye hii bill.
Mimi siwezi kusema kwamba naipinga. Nachowezatu kusema ni kwamba sielewi kwa nini iwe kosa kwa Mgombea Urais kupokea msaada kutoka nje ya Nchi siku tisini kabla ya Uchaguzi. Kwa sababu nimeufuatilia huu mjadala katika Bunge,na hili ndilo lililosemwa,kwamba Mgombea Urais anaweza kupokea msaada kutoka nje,lakini iwe siku tisini kabla ya Uchaguzi. Kwamba jkatika miezi mitatu ya mwisho ya Uchaguzi haruhusiwi kupata msaada kutoka nje. Kwamba Serikali inapinga kabisa ile last minute help.
Mimi sielewi kwa nini iwepo sheria kama hii,kwa sababu ukitazama story nyingi za Uchaguzi utaona kwamba many a campaign has been helped by a last minute spurt of energy and money.
Kama Kikwete ndiye atakayekuwa Mgombea Urais wa CCM,sheria kama hii itamlinda Kikwete,ita,linda mtu yeyote nchini ambaye anazo hela tayari.
Tumekuwa tunaongea siku zote tunasema kwamba safari za Rais kwenda Nje zimezidi. Kwa nini basi Rais anahangaishwa na watu toka nje kuwal;etea msaada watu wengine na siyo yeye.? Ina maana Rais akienda huko nje mara nyingi,haisaidii kupata rafiki wengi?
Mimi siyo mtaalamu wa sheria,na maswali swali ambalo naweza kuuliza kuhusu sheria hii,au sheria yoyyte nyingine ambayo itapitishwa na Bunge,ni kwamba,inalingana vipi na sheria zingine katika Nchi nyingine? How does it compare to the election law in America or elsewhere? Kwa sababu,Campaing Finance Reform,maana yake kwamba mtu hapaswi kuleta fedha chafu katika Kampeni,yaani fedha alizozipata katika biashara ya watumwa. Au fedha za Kampeni zisizidi kiwango fulani,yaani kiwango kikubwa sana kuliko gharama za usafiri,au gharama za accomodation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…