GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Wala sitaki Kuzunguka sana katika hili ila miaka mitatu minne iliyopita wakati nikiwa busy na masuala ya Mpira hasa huu wa Bongo ( VPL ) kupitia Klabu yangu pendwa kabisa ( ambayo kila Member humu anaijua ) niliwahi kufanya mambo mengi ya ' Kumkufuru ' Mungu ili Timu yangu hiyo ishinde japo tuliangushwa mara kwa mara na Kiongozi wetu mmoja ambaye sasa ana Kesi na yupo Lupango akisubiri hukumu yake kwakuwa alikuwa akitumika na upande wa pili ( Wapinzani Wetu ) akitumiwa sana na ' Tajiri ' wa zamani wa hiyo Timu aliyefululiza kuwa na ' Kesi ' mwaka jana hadi kupelekea Mimi GENTAMYCINE kukaa pembeni na Soka la Bongo kwa muda mrefu.
Kuna ' Kashfa ' moja nimeisikia leo ya ' match fixing ' ambayo imewahusisha Waamuzi wetu ila Mimi kwa uzoefu wangu na harakati zangu katika Soka la Bongo nitamzungumzia mmoja wao tu hapo ambaye nilimfahamu vyema na mara nyingi ' nyendo ' zake ambazo zinafanana na hizo alizotuhumiwa nazo huko Rwanda nilizijua vyema tu.
Naandika haya nikijua na nikiwa na uhakika wote kwamba hata wale Watu wa mpira wenzangu ambao mara nyingi huwa tunakuwa karibu na hizi Timu kubwa mbili hivyo haya nitakayokuwa nayaeleza hapa hawatakuwa wageni nayo sana labda tu waamue ' kuyachunia ' ili kuyaficha ila Mimi nitaweka yale ambayo nayajua.
Kwa Mtu wa Mpira yoyote hasa wa hili Soka la Bongo ( VPL ) hakuna asiyejua kuwa ' tatizo ' kubwa la huyu Mwamuzi Israeli Mujuni Nkongo ni kupenda sana kuchukua ' rushwa ' Sisi Watu wa Mpira tuna msemo Wetu ambapo huwa tunasema kuwa ni Mtu wa ' mbili kwa nne ' sana na bahati nzuri hata Yeye mwenyewe alifika hatua akawa hajifichi.
Niliweza kumjua mno Mwamuzi Israeli Nkongo na hasa kuhusu tabia zake hizo za kupenda ' Milungula ' au ' mbili kwa nne ' hasa pale alipokuwa anatumika wazi wazi kabisa kuibeba Klabu moja Tajiri iliyopo Mbagala hadi akafanikisha kuwa Bingwa katika miaka michache iliyopita na hakuishia tu kupewa hizo Hela bali kuna hata ' zawadi ' fulani fulani alipewa kama sehemu ya ' Fadhila ' kutoka kwa hiyo Klabu.
Nina Rafiki yangu mmoja ambaye ni Dereva wa Gari la Waamuzi ( jina nalihifadhi ) hapa Mkoa wa Dar es Salaam niliyetokea kujenga nae Urafiki kiasi kwamba mara nyingi hata katika maongezi yetu alikuwa akinithibitishia tabia za Mwamuzi Israeli Nkongo na Mwamuzi mwenzake mwingine ambaye Jina lake la Ukoo linaanzia na herufi ' C ' na pia ni Askari ( ila siyo wa JWTZ )
Nakumbuka kuna siku ilikuwa mechi ya Timu yangu pendwa inacheza na hao ' Matajiri ' wa Mbagala ambapo kama kawaida siku hiyo nilikaa pale pale VIP B nikiwa jirani kabisa na huyo Rafiki yangu ( Dereva wa Gari la Waamuzi / Marefarii ) ndipo kwa kuniamini kabisa kabla hata Timu bado hazijaingia pale Uwanjani ( Taifa au kwa Mchina ) kwani nilikuwa na tabia ya kuwahi kuingia ' Jamaa ' akampigia Simu Mwamuzi Nkongo na kuweka ' Loud Speaker ' na akaanza ' kumchomekea ' hiyo mechi ambayo alikuwa anaichezesha ndipo Nkongo bila haya wala aibu akazungumza Kauli ambayo hadi leo naikumbuka na sitoisahau ambapo alisema nainukuu..." Hao Simba Washamba sana Kaka wenzao wa Mbagala walishanicheki mapema tu ila Wao wanajifanya kuwa Wabahili sasa ngoja leo niwaonyeshe labda siku nyingine wataamka " na nakumbuka hiyo mechi Timu yangu hiyo pendwa ilifungwa na hadi akampa Kadi Nyekundu mchezaji wetu mmoja muhimu wa Kiungo.
Na mchezo wake huo huo aliendelea nao hata katika mechi moja baina ya hao ' Matajiri ' wa Mbagala na Wamiliki wa Bwawa Kuu la Kuogelea Jangwani ambapo ' aliwauma ' sana wenye Bwawa la Jangwani kiasi kwamba ilipelekea hadi Wachezaji wake ' Kuhamaki ' na mmoja wao aitwae Stephano Mwasika kuamua Kumpiga bonge la Ngumi la Usoni Mwamuzi Nkongo ambayo ilimpata kisawasawa hali ambayo ilifanya alazimike kufanya kila awezalo ili mechi ile iishie kwa Sare ( Draw ) ili Kuokoka na ' Kipigo ' cha ' Shalubela ' ambacho alianza Kukiona kinamjia na kweli mechi ile iliisha kwa sare ya 3 kwa 3.
Iwe isiwe kwa kilichotokea huko Rwanda na kwa hatua ambayo CAF wameichukua dhidi ya huyu Mwamuzi na jinsi ninavyomjua ' Kindakindaki ' nina uhakika kwamba anaenda kututia aibu Watanzania kwani nahisi 98% Uchunguzi ukifanyika kwa umakini wote lazima tu atagundulika kuwa ' alihongwa ' huko nchini Rwanda alipokuwa akichezesha hiyo mechi ya Rayon Sports na kama akipona katika hili basi ushauri wangu mkubwa mno GENTAMYCINE kwa Israeli Mujuni Nkongo ni kumtaka tu aachane na kuwa Refarii / Mwamuzi na afanye shughuli zake zingine.
Nawasilisha.