Hata kama Dkt. Tulia unakubalika Mbeya lazima uambiwe ukweli. Kipindupindu Mbeya ni ukosefu mkubwa wa maji

Hata kama Dkt. Tulia unakubalika Mbeya lazima uambiwe ukweli. Kipindupindu Mbeya ni ukosefu mkubwa wa maji

Mpap Ndabhit

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
331
Reaction score
416
Mbeya shida ya maji ni kubwa kuliko wanasiasa wanavyojua. Labda Kipindupindu ndiyo kitawaumbua. Pamoja na miradi mikubwa Mbunge Tulia ameileta Mbeya ukweli mradi wa maji umechelewa. Watu watakuwa wamekufa na Kipindupindu.

Suala la Kipindupindu Mbeya halihitaji utafiti. Jibu liko wazi Mbeya wanakunywa na kutumia maji ya vyooni. Ni kawaida maji kutotoka kwenye mabomba zaidi hata ya mwezi. Maji yanayotumika ni maji ya visima katika nyumba zilizosongamana.

Hayo ndiyo wananchi wanakunywa, kuoshea vyombo, nk. Jiji Zima la Mbeya. Mtu alikusudia kuchimba shimo la choo.sasa wakati anajipanga kukamilisha choo majirani wanatumia Kwa matumizi ya nyumbani. Rangi ya maji hayo ni njano.

Kabla ya kufungia visima ningeomba tatueni changamoto hii ya maji najua Kipindupindu kitaishia hapo. Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom