Hata kama huna vyote haujanyimwa vyote

Hata kama huna vyote haujanyimwa vyote

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nyoka hana miguu wala mikono, lakini halali njaa, na anatumia sumu yake kama silaha ya kujihami dhidi ya maadui zake!

Kinyonga hana uwezo wa kupambana na viumbe wakubwa, lakini kwa uwezo aliojaliwa wa kujibadilisha rangi humfanya asionekane kirahisi na viumbe hatarishi kwake

Tembo ana nguvu kumzidi mwanadamu, lakini mwanadamu, kwa kuwa ana akili kuwazidi wanyama wote, ameweza kuwa mtawala wa viumbe vyote, Simba na Tembo wakiwemo.

Karibia kila binadamu anahisi anapungukiwa kitu fulani maishani mwake, lakini hakuna mtu asiyekuwa na kitu.

1. Nimeona wana ndoa ambao pamoja na kuwa wasomi na matajiri, watoto wao waliishia kuharibikiwa. Walifanikiwa kielimu na kifedha lakini wakafeli katika malezi ya watoto wao.

2. Nimeona watu ambao ni walevi na masikini, lakini wakawa na watoto wenye tabia njema na mafanikio kifedha, n.k. Pamoja na umaskini na ulevi wao, walifanikiwa kutaokuwaambukiza watoto wao hizo tabia. Walifanikiwa katika malezi.

3. Wanasaikolojia wanadai kuwa mtoto aliyelelewa na mzazi mmoja huweza kuwa na upungufu Kisaikolojia. Kwa niliyoyaona, ninathubutu kusema hawako sahihi kwa asilimia zote. Kuna watu wamelelewa na mzazi mmoja, na wengine wamelelewa na watu wasio wazazi wao wa damu, lakini wakaishia kuwa watu "wazuri" wa kupigiwa mfano katika Jamii, hata kuwazidi waliolelewa na wazazi wao wa damu.

4. Nick Vujicic alizaliwa bila miguu na mikono. Lakini ana mke mzuri, watoto wazuri, nyumba nzuri, gari zuri, furaha na fedha nyingi kiasi cha kutoa misaada kwa wenye uhitaji.

Usinung'unike kwa sababu unahisi kuna ulichopungukiwa. Huenda huo ni mtazamo wako tu.

Kuna ulicho nacho ambacho pengine mwingine hana. Itumie kikamilifu. Itakufikisha mbali.
 
Attachments

  • Nick_Vujicic_s_Life_Without_Limbs(144p).mp4
    2.8 MB
  • Nick_Vujicic_s_biography(144p).mp4
    5.2 MB

Shukrani kwa bandiko murua
 
Bandiko safi sana mkuu.
Linatufundisha umuhimu wa kushukuru na kupambana
 
Wakati wewe unajiuliza wamewezaje, mwenzako anajiuliza umeshindwaje.

Unapolalamika hauna viatu, kuna wenzako hawana miguu.... na wanamshukuru Mungu.
 
Back
Top Bottom