Hata kama ni MC wa kukodi, kwanini akodiwe mtu aliyefungiwa?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Bado sijaelewa hili jambo , ilidaiwa Manara kafungiwa asishiriki shughuli za Soka za ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili , sasa leo kaonekana kwenye tamasha la Yanga , KWA KISINGIZIO CHA MC WA KUKODIWA , na baada ya kumaliza kuwatambulisha wachezaji wa Yanga , Manara amedai kwamba hajihusishi na soka na anaondoka kwenda huko Kigogo kufanya shughuli zake za UMC kwenye harusi .

Hili jambo limekaaje jamani ?
 
We mbumbumbu unaumia ukiwa wapi?
 

Hapo Yanga wamekosea, Hakukuwa na sababu ya Manara kuwa MC leo.
 
Mpeni jamaa nakala ya hukumu hayo yote yataisha . Nakala ya hukumu hamtaki kumpa mnahofia atakata rufaa . huku kanuni zenu zinasema adhabu itaanza kuhesabika Mara tu mtuhumiwa anapopewa nakala ya hukumu. Mnajikaanga kwa mafuta yenu.
 
Aongzewe mwaka wa tatu!
 
Huyu ban ya maisha inamuhusu..Ameidharau taasisi nampira wa bongo na ameifanya taasisi km haina meno na haing'ati
Shughuli siyo ya TFF, na sidhani kama Yanga wameomba kibali TFF kufanya shughuli Yao ya kutambulisha wachezaji, watakuwa wamewafuata DRFA kwa ajili ya mechi ya saa 1 Usiku!!!
====
Ni mwendo wa kuvurugana tu hakuna namna!
 
Hapa Yanga wakiadhibiwa na TFF watasema wameonewa. Ki ukweli Yanga ni kubwa zaidi akili na jina la Manara. Kuna haja ya viongozi wa timu kutoingiza timu kwenye migogoro na mamlaka za soka na michezo kwa cheaper reasoning eti, 'mc'

Huu ni ukaidi, ipo siku Manara atamshika 'kalio' hadharani Injinia Hersi au Ghalib Said ndio wataona faida ya adhabu ya TFF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…