Itenda Jimmy Joyce
Member
- Aug 17, 2022
- 10
- 2
KUFELI ni kushindwa kukamilisha jambo kwa wakati. Husababishwa na hofu, kukosa uzoefu au kukosa kujiamini. Hakuna mafanikio bila maumivu, hata mbegu hulazimika kuiumiza ardhi kwa kuipasua ili itoke.
Hivyo kijana unapofeli, badala ya kulalamika, kujiona huwezi hata kutafuta mtu wa kumlaumu au kujilaumu mwenyewe, simama kwa ujasiri na ujiambie mwenyewe MIMI NI MSHINDI. Hata kama mbele yako unaona giza bado tambua kuwa kuna chini yako kuna ardhi inaweza kuwa daraja lako ikanyage na upige hatua kuelekea mbele, hata kama mbele unaona shimo na ndani yake kuna matope(changamoto) jipe moyo hata kama utaanguka tambua kuwa hayo matope ndiyo yatakushikilia ili usiendelee kuzama, utainuka na kuanza tena huku ukisahihisha makosa.
Amini kuwa siku moja utakuwa siku moja makosa yatakuwa shuhuda juu ya mafanikio yako. Maana huwezi kuutambua uimara pasipo kuujua udhaifu na hasara huitambulisha faida. PAMBANA TU! Wewe ni SHUJAA
Hakuna aliyezaliwa kuwa tegemezi, bali kujitegemea na kutegemeza wengine ili nao siku moja wasimame peke yao. Kinachotakiwa ni kujijengea imani kuwa MIMI NI MSHINDI hata kama
-Familia ni maskini.
-unahistoria mbaya.
-umefeli mara nyingi.
-hujasoma.
Lakini kuna kitu ambacho hakichakai ni "AKILI" Hicho pekee kinaweza kuwa mtaji wako mkubwa na nguvu kukuwezesha kuanza upya.
Tambua kuwa kuna eneo lako au kitu ambacho hakuna anayeweza kufanya zaidi yako ndiyo maana ulizaliwa la sivyo hakukuwepo na sababu ya wewe kuzaliwa, inawezekana lipo tayari au unasubiriwa wewe ukianzishe ili lianze kuwepo juu ya nchi.
Thamani yako inapaswa kudhihirishwa katika matendo na siyo maneno pekee, maana maneno hupotea bali matendo huonekana na kukaa. Na mbegu ili ipaliliwe ni lazima iote na juhudi za kuota siyo za mpandaji bali ni za mbegu yenyewe kupambana kupasua ardhi ili ionekane, kisha mkulima huja kupalilia na ile iliyoshindwa huoza na kuwa mbolea kwa ile iliyomea.
Hivyo kijana acha kujiona upo pekee yako bali simama uanze ili watu waone jitihada zako ndipo watakapo shawishika kukushika mkono na kukuimarisha zaidi hata utakapopata nguvu za kusimama mwenyewe.
Amua kuwa MBEGU bora simama uanze maana WEWE NI MSHINDI.

Upvote
0