PreGE2025 Hata Kusipofanyika Reforms, 2025 CHADEMA Ina Fursa!, Ila They Are Just Too Blind to See!, Hawajitambui! No Election ni Utopia!. Wake Up!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wasusie tu ni haki yao
 
Mimi najiuliza ccm hawana vijana wasomi mpaka wampendekeze mzee wasira na makala? Hao niwachumia tumbo tu, watanzania tuamke wakati wa Mungu ndio sasa. Kwa pamoja tuiunge mkono chadema.
 
Nmekuelewa sana Pascal mwaka huu hata mimi naona kama kuna kamseleleko kwa upinzani kama tu Chadema wakikaa pamoja wakaelewana kuingia mazima wakaacha tabia za kususa, Mana naona karibu TOP yote ya sisiem haina mvuto kwa wananchi na pia wananchi wengi hawawazungumzii vizuri zaidi ya CHAWA wa mama. Kwa kifupi wananchi hawana matumaini na TOP leaders. Bila gori la mkono sisiem hawatoboi.
 
Hivi kuna mserereko zaidi ya uchaguzi wa vijiji, vitongoji na mitaa?

Yaliyotokea kila mtu anajua

Babu yangu aliniambia
Kurudia kufanya kitu katika mazingira yanayofanana na kutarajia matokeo tofauti ni upunguani!
 
Nakushauri Bwana Mayala gombea Tena ubunge wa Kawe CCM, ukishinda ubunge na kuapishwa ndipo utapata uhalali wa kuishauri CHADEMA. Wewe Jimbo la Kawe jijini Dar limekushinda utamshauri nini Lissu aliyekuwa mbunge huko vijijini tena Singida kwa vipindi viwili? Karibu kuwa realistic saa zingine.
 
Binafsi naona ubinafsi umetawala kwa uongozi mpya, ningeshauri kwanza viongoz wa sasa na zamani wakaitana wakaombana msamaha kwa yote yaliyopita, na kuwaunganisha wanachama kuwa kitu kimoja, bila hivyo uongozi mpya una kazi kubwa ambayo naiyona inaendq kuishia njiani, yanayofanywa sasa na uongozi mpya nikama kutaka kumuonyesha kiongozi kwamba nawao wanaweza, kuliko kuangalia umoja wa chama
 
Kama akina Chief Mkwawa, Wangekua na Akili kama hizi za akina Pascal Mayala. Basi Tungekua utumwani mpaka mwaka 2001.

Binafsi sina Chama, Lakini kama Tume ndo hii. Mimi siku ya Kupiga kura hamnioni hata mnilipe.
 
Advocate, Hizo Reforms ni Faida hata kwako.
Utamchagua mtu umtakaye sio wanaemtaka wao.
 
Duh 🙄 !
Kwenye Uzi huu zinatolewa Nondo sio za mchezo mchezo tena zilizokwenda Skuli kweli kweli !
Sina la kuongezea !
Ngoja Tusubiri tuone. ! 😳
 
No reforms No election ndio habari ya mjini kuanzia sasa hadi mwaka huu uishe. Hii miruzi mingi inayopigwa hasa wakati huu, haipaswi kumchanganya Lissu na CHADEMA yake. Nashauri akamatie hapo hapo ikiwezekana aongeze kamba zaidi juu ya kabari kwa kuwa wananchi wameanza kuelewa. #Chochea Moto Uwake#
 
Huwa najiuliza kijiswali kidogo tu, Kwanini CCM hawataki kusikia kuhusu haya mabadiliko wanayotaka CHADEMA? kwamba wanajua wanashinda kwasababu tume ni yao na wakifanya mabadiliko watapigwa chini au kuna lingine? Mwenye kujua anifahamishe

Wanajua hua hawashindi kwenye box la kura, Ndo maana kukubali haya Mabadiriko ni kukitia chama Motoni.

Lakini kila kitu kiko na Mwisho. Sijui kwann hawajipangi kwa huo Mwisho.
 
Wanajua lakini hawataki kusikia majuto mjukuu. Asiye pata kura za kutosha ndiye anaye pitishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…