PreGE2025 Hata Kusipofanyika Reforms, 2025 CHADEMA Ina Fursa!, Ila They Are Just Too Blind to See!, Hawajitambui! No Election ni Utopia!. Wake Up!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
You are telling them they're blind. I think you are out fashioned. Please shut up or choose to support your garbage party. Unakataa reforms kweli? Wewe unaona haina tija? Unagombea Urais,unashindana na Rais ambaye ndiye amemteua mkurugenzi wa tume ya uchaguzi na waandamizi wengine. Wewe kwako unaona ni sawa hiyo? Ulipoteza muda shuleni
 
CDM ilianza na wabunge wachache 2015 na moto wao Bungeni uliuona walichorespond CCM kwenye chaguzi za 2019, 2020 na 2024 umeona ...

miaka hii ya mama kuna madudu mengi sana yamefanyika, wakiingia watu makini bungeni patachimbika!

ndiyo maana wameona heri wawaondoe kabisa wapinzani bungeni
 
Hata kusipofanyika reforms, uchaguzi wa 2025 CHADEMA ina bonge la fursa!,
Mkuu,tunakuheshimu sana kuanzia vipindi vyako ukiwa channel ten TV,na kuendelea hakuna asiyejua umakini wako
ila linapokuja suala la siasa huwa unatuangusha sana. Nilidhani labda unavizia teuzi lakini nikaona wanapita viongozi wengi huteuliwi kwenye nyadhifa basi nikadhani labda uwa unazikataa sina majibu.

Ni nani ambaye hakuona fursa ya NCCR mwaka 1995, na tukadhani nchi inapata uongozi mpya kila mtu anajua kilichotokea
Njoo 2015 ambapo wengi tuliamini kuwa utabiri wa mwalimu unatimia kwamba mpinzani wa chama tawala atatoka mle mle mle,tunajua yaliyotokea. Alipoingia mh.magu ikulu binafsi alinifungua macho kwa bifu alilolianzisha na wapinzani mwenye macho na moyo wa ufukunyuzi alijiuliza aliikuta siri gani huko?
Leo tukisema kuna fursa,itakuwa ni kujidanganya bila kubadilisha mifumo iliyotenda kazi hadi fursa zilizowahi kujitokeza zikapotea.
wote sasa hivi tunaimba NO REFORMS NO ELECTION kama fursa uliyoiona itapotea,haitakuwa ya kwanza kupotea.
 
Mbona huwa huongelei lolote kuhusu mazingira ya uchaguzi kama yako sawa kwa wote.
Je,ni kweli CCM hawana upendeleo wowote kwenye michakato ya uchaguzi?
 
Ushauri wa watu wa aina yako ndiyo umekifanya CCM kidumae, kuwafanya viongozi miungu wenu na hata wanapoiharibu nchi, wasishaurike kwa manufaa yao binafsi. Matatizo ya watanzania yanasababishwa na ubinafsi wa wachache wajanja wanaonufaika. Siku zote hamtopenda kila mtanzania afikie matawi mnayokula. Chadema inapowaamsha wananchi wakwee juu kwenye matawi mnayokula kamwe hamtofurahi, lazima mlinde ugali wenu. waache wapambane na dhulma ya ccm, ushauri wako peleka ccm kwa wakondesha nchi wenzio.
 
Duh 🙄 !
Wakondesha Nchi 😳😂😂😂 !
 
"NRNE ni Mpango wa Shetani, ni li Pepo! Limemkumba Lissu!, Akiachana Nalo, Anatinga Ikulu 2025!"

Kwa kiswahili sanifu Pascal Mayalla anasema, Bila reforms Lissu anashinda Urais akigombea.
Mkuu Msolo , karibu
mitaa hii,
Huyu Jamaa akitia timu
yaani ni saa 4 tuu asubuhi! Kazi kwisha!
P
 
Maandiko yako Kaka Mkubwa huwa ni Marefu sana asee! Kuisoma yote labda uandike barua ya likizo ili muda utoshe kuisoma. Jitahidi kuwa unaandika kwa vipande vipande kiongozi. Nimeshindwa kuimaliza ...Ndefu mnoo. Hata vitabu vinaandikwa kwa Sura au Topic kaka. Ni ushauri
 
Chadema walishiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa walipata nini miaka 60 ya Uhuru bado watu wanaendekeza siasa za kitapeli nchi za afrika kupata maendeleo ni kazi sana maana tunapata Viongozi ambao hatuwachagui ndo maana wanajawa na kiburi na dharau wakienda Bungeni baada ya kusimamia Serikali itimize uwajibu wake wanageuka kuwa wapambe wa serikali kwa staili maendeleo sahau
 
makosa ya 2019, 2020 na 2024 CDM wasirudie tena,

kawa maFISIEM yamejipanga kuiba kura yakajiibie yenyewe na sio CDM kutumika kuhalalisha wizi wa kura.
 
Maelezo meengi embu waambie CCM waweke tume huru ya uchaguzi na katiba ya kidemokrasia then uinange CDM
 
Kulikua na shida gani kusema ni mwanachama wa sisiemu? Tunashindwa kutoa maoni kwakua hatujui unayafanya haya ili iwe sympath urudishiwe tender zako za PR au lakini tunakuonea huruma wewe kwa uliyofanyiwa na unavyo behave.
 

Attachments

  • 20250523_062918.jpg
    52 KB · Views: 22
Paskali upon humu tangu miaka jukwaa linaanza sidhani kama Kuna Uzi wa kuhamasisha watu kupiga kura 2010,2015, labda 2020.

HIKI kinachotokea Hadi Sasa Mimi sikielewi, maana enzi hizo hata angetokea mtu anasema tusipige kura Bado tungepiga na tume ilikuwa ni hiihii. Tatizo ni nini?
[/QUOTE]
Karibu mitaa hii
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…