Hata mbuyu ulianza kama mchicha

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2019
Posts
8,447
Reaction score
19,425
Nimekuwa nikisikia hii kauli toka nikiwa mtoto hadi leo. Ni kauli inayotolewa kama kutia moyo, kurudisha morali iliyopotea/kuelekea kupotea au kusifu pale unapofanya kitu au kufikia mafanikio fulani baada ya kupambana na kusota kwa muda fulani. Ni kauli/msemo fulani wa kawaida ambao sijui unabaki kuwa tu kama misemo na nahau zingine au ni kweli kwamba mibuyu yote tunayoiona iliwahi kuwa midogo saizi ya mchicha kipindi inapita hatua mbalimbali za ukuaji.


Kila nikiusikia huu msemo hua napata mkanganyiko wa fikra kidogo maana kwa umri nilionao, kusafiri sana hasa mikoa ya katikati mwa Tanzania ambamo ndo hii miti inapatikana kwa wingi ila pia kuangalia picha na kuangalia sana chaneli za mambo ya wanyama na mimea nikiri kwamba sijawahi kubahatika kuuona huo mbuyu unaolingana na mchicha. Yote nayoiona inakuwa tayari ni mikubwa saizi ya kibanda.

Nimekuja jukwaa hili kuomba kama kuna yeyote aliewahi kuona mbuyu unaolingana na mchicha achangie hapa ujuzi na kama atatuwekea picha hapa au akaelekeza wapi naweza kujionea kwa macho mbuyu unaolingana na mchicha itapendeza sana. Mi imefikia hatua naanza kuamini haya mamiti yalishushwa hivo hivo yalivo ila pia najipinga mwenyewe kama yanatoa mbegu si maana yake zinaota na kama zinaota utotoni mwao si lazima tu yatalingana na mchicha. Au ndo zile habari za nyangumi kuzaa mtoto analingana na nyati dume kubwa la kundi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…