Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Magulumangu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
3,051
Reaction score
461
Nitaanza kuwataja,kwa majina na tabia,
Afrodenzi namtaja, nyamayao fatilia,
Nilham anakuja,wa rasheedi fatilia,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Judi wetu mwanaheri,asha d sitokuacha,
sweetlady yu mahiri,lizzy ye muarusha,
Brackberry stahiri,kukuacha tutaisha,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Mwanajami1 jamani, jukwaa liwakilishe,
Pearl Matty huerini,Kareen_hapuch miche,
Daughter wake zioni,Blaki woman turushe,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Sio kwamba nakuacha, hili ni duru la kwanza,
Mkao kula kukicha,ntakuja na wa kwanza,
Wewe mwana maisha, kwa jina lake ni minza,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,
 
Hahhahhah Lizzy sio Muarusha bwana!!!
Ila kitu kimetulia!Endelea.....
 
Hahhahhah Lizzy sio Muarusha bwana!!!
Ila kitu kimetulia!Endelea.....


lizzy wewe hukumbuki, ulopita niambia,
mimi sio mamuruki,kusahau lipoanzia,
unga ltd hukumbuki,kwenu lishaniambia,
Kumbuka lichosema,isije kuwa ajali.....
 
too biased........majina yote ya wabeijing!!!!!!
 
Hivi mastaa wako hakuna wa kiume? Mbona wote wa kike?
 
lizzy wewe hukumbuki, ulopita niambia,
mimi sio mamuruki,kusahau lipoanzia,
unga ltd hukumbuki,kwenu lishaniambia,
Kumbuka lichosema,isije kuwa ajali.....
Magulumangu jamani mbona wataka niumbua..
Nilichokwambia sirini hadharani wafichua....
Kila nililokueleza hivi sasa najutia....
Hakika nakwambia leo mwisho kunijua.,,
 
too biased........majina yote ya wabeijing!!!!!!

usiwe sana muwewe,kudandia basi mbele,
soma pasipo kiwewe,nielewe yangu pale,
nimesema hata wewe,la kwanza duru kihele,
Ukiwa mkimya bora,kuropoka bila kujua,
 
kweli 2po ktk zama za sayansi na teke linalokujia,yaani mpaka Star nazo ni memba wa jf na zinaweza kuandika Kiswahili!
 
kweli 2po ktk zama za sayansi na teke linalokujia,yaani mpaka Star nazo ni memba wa jf na zinaweza kuandika Kiswahili!


Washawasha ntakuja,unikune kule kunako,
tutaenda mpaka unguja,tupitie na moroko,
heri yeye mkunja,salimia nakonako,
Wasalimie joburg,soweto pia wape hai,
 
Magulumangu jamani mbona wataka niumbua..
Nilichokwambia sirini hadharani wafichua....
Kila nililokueleza hivi sasa najutia....
Hakika nakwambia leo mwisho kunijua.,,


Msamaha na uwepo,mama nilishapitiwa,
Mwanzo wetu si pepo,kwake maombi mpendwa,
Haukuja kama upepo,hakika lifunuliwa,
Pole yake mama pole,kobe mbali husafiri,
 
mmmmh, wewe mtoto una hila weye...lol.....

nilimjaribu nyuki,kumbusu nikakoma,
nilidhani yu hayuki,asali yake huuma,
ustaa sio mbuki,kutaka kwa huruma,
Asante mwana kuona, yake hila jamaa,
 
Nitaanza kuwataja,kwa majina na tabia,
Afrodenzi namtaja, nyamayao fatilia,
Nilham anakuja,wa rasheedi fatilia,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Judi wetu mwanaheri,asha d sitokuacha,
sweetlady yu mahiri,lizzy ye muarusha,
Brackberry stahiri,kukuacha tutaisha,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Mwanajami1 jamani, jukwaa liwakilishe,
Pearl Matty huerini,Kareen_hapuch miche,
Daughter wake zioni,Blaki woman turushe,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Sio kwamba nakuacha, hili ni duru la kwanza,
Mkao kula kukicha,ntakuja na wa kwanza,
Wewe mwana maisha, kwa jina lake ni minza,
Hata sisi ni staa, kwa majina nitataja,

Ai ai ai ai ai ai,...
so siku hizi watu wa TRC kazi yenu ni kuandika mashairi tu?
ops,kumbe sipo kwenye siasa,...
mashairi bomba sana mkuu
 
Ai ai ai ai ai ai,...
so siku hizi watu wa TRA kazi yenu ni kuandika mashairi tu?
ops,kumbe sipo kwenye siasa,...
mashairi bomba sana mkuu

Vipi tena mkuu? Naona Anna Makinda anakuudhi sana mzee, TRA wapi tena? Hapa mapenzi mkuu hahahahahahahhahahaha.....
 
Back
Top Bottom