Lazima tukubali kuwa Mustakabari wa katiba mpya upo mikononi mwa wabunge wa CCM. Wingi wao unatishia kila uamuzi unaotumia kura.
Ndo mana wengine tunataka kura ya siri tukiamini kuwa kuna wabunge wa CCM watapata nafasi ya kuchagua kinyume na matakwa ya CCM.
Kosa lilishafanyika kuruhusu wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano na wajumbe wa baraza la wawakilishi la zanzibar wawe wajumbe wa bunge maalum la katiba, badala ya kuweka idadi sawa ya wajumbe kwa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu.
Kutenda kosa si kosa, kosa kurudia kosa.
Tupaze sauti zetu, kalamu zetu, nyimbo zetu, maigizo yetu na kila nyanja ya fasihi juu ya katiba tunayoitaka ili wabunge wengi wa CCM waelewe umuhimu wakuwa na katiba bora na siyo bora katiba. Tukiweza hilo ndipo tuakapo kuwa na uhakika wa kupata katiba ya wananchi