Hata usipooa au kuolewa hutakufa………!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Watu wengi sana ambao hawajaoa au kuolewa huwa wanafikiria zaidi kuhusu kumpata mtu anayefaa. Wanawake ndio wako kwenye kifungo hiki zaidi. Jamii imewaambia kwamba, umri unavyoongezeka na nafasi yao ya kuolewa na pia kuzaa watoto inakuwa finyu zaidi. Kwa bahati mbaya wameamini hivyo.


Lakini nijuavyo mimi, maumbile hayana kuoana, wala hayana kitu kinachoitwa watoto wa nje ya ndoa. Najua kauli yangu hii itawakera wale wanaoamini katika dini zao hizi za mapokeo, lakini huo ndio ukweli wenyewe.

Lakini naamini watakubaliana na mimi kwamba, hata waanzilishi wa hizi kubwa, sio wote ambao walioa. Ingekuwa kuoa ni suala la maumbile, basi nao wangeoa pia. Ukweli ni kwamba kuoa au kuolewa ni suala la binadamu zaidi. Hivyo uoe au usiolewe ukweli kwamba utabaki kuwa binadamu na kutimiza kile kilichokuleta duniani, hauwezi kuondoka.
 
kadadeki ebu ngoja upate ajali alafu uparalyse alafu uwe hujaoa au hujaolewa uone matusi utkayoporomoshewa na ndugu zako
oh mie sioi sasa ona unvyotapatapa...nani aje ashike mavi yako hapa.

tusidanganyane kuoa ni muhimu upende usipende. wale ambao wataki kuoa basi wafanya moja kati ya haya
1) hakikisha unapesa za kutosha kiasi cha kwamba ukizeeka wewe unaenda old mans home
2) kuwa na bunduki yako pembeni kabisa na uwe na mentality ya kwamba kama likitokea lolote najipiga risasa. hujafa hujaumbika kaka lolote laweza tokea na wakaribu yako ni mke/mume ndugu watakuja leo na kesho ....binadamu achelewi kuchoka!!! na juu ya hapo watakumwagia matusi.
 

Mkuu, Umeona mbali sana tena kwa upeo wa Darubini Thankx.
 
Mzabzab, maneno yako yamenigusa, haswa hapo pa "ndugu kuchoka". Nimeshaona kesi mbili za namna hiyo. Inabidi nifikirie mara mbili. Hujafa hujaumbika! Yakinikuta ntakuwa mgeni wa nani mie? Eh Mungu ninusuru.
 
Mtambuzi labda tuanzie hio sentensi yako ya mwisho.... Ni nini hasa kimetuleta hapa duniani na wajiibu wetu ni upi??
 
Kweli!! Lakini kuna raha unakosa bana.
 
Mtambuzi labda tuanzie hio sentensi yako ya mwisho.... Ni nini hasa kimetuleta hapa duniani na wajiibu wetu ni upi??

Mungu ametuweka duniani tumjue, tumpende, tumtumikie, tupate kufika kwake mbinguni!!!
 

wanaume wanaooa kwa sababu kama zako sidhani kama wake zao wanafurahia ndoa.
 
mhm usipo mfurahisha mkeo ukipatwa na majanga unadhani anakaa?
wote unaona wanakaa ujue kweli mwanawane alikuwa anamjali.
 

weeeeeeeeeeeeeeeeeeee! ishia hapo hapo! tuseme ndo unamuombea mgonjwa mabaya au hujui yalo msibu Baba Ngina eeeeeeeee! Ushindwe kabisa kumuombea mgonjwa ugonjwa zaidi, lol, shetani na ashindweeeeee!
 
Mtambuzi labda tuanzie hio sentensi yako ya mwisho.... Ni nini hasa kimetuleta hapa duniani na wajiibu wetu ni upi??

Kuna Mwalimu wangu wa Ekolojia aliwahi kusema kwamba binadamu yuko duniani kwa ajili ya kazi kubwa mbili tu, ambazo ni:

1. Kuishi maisha ya kumpendezesha yeye na jamii anayoishi nayo,
2. Kuzaa then kinachofuata ni kifo tu.

Tafsiri ya imani ya kidini, naomba muitoe nyinyi

Mengine yote ni vikolombwezo tu vyamaisha, kimsingi uwepo wako duaniani una maana zaidi ukiyatimiza hayo mawili. Ndiyo maana kule usukumani ukifa bila kuacha mtoto, kaburi lako halijengewi, linaachwa kama tuta la viazi ili baadae lipotee kabisa maana hukuwa na maana yoyote ya kuja duniani, hakuna kumbukumbu yoyote uliyoacha ili hali mungu alishasema nendeni mkazaane muijaze dunia!
 

Ndoa ndio inayotutofautisha na wanyama Mkuu la sivyo watu wangepanda dada zao bila kizuizi
 

nilijua kuna watu watakuja na mtazamo huu..... hukusoma na kuelewa mada yangu, au niseme uliitafakari kutokana na mazoea. kama ungekuwa umeisoma na kuitafakari kwa jicho la tatu, naamini isingekupa shida. ingawa wapo waliokwishakujibu, lakinisina budi kuweka angalizo.
naamini utakubaliana na mimi kuwa wapo wanaume na wanawake ambao wameingia kwenye ugigili (frustriration) kwa sababu ya kujikuta hawajaoa au kuolewa na umri kuonekana kuwatupa mkono. nilibainisha kuwa wanawake ndio wako kwenye kifungo hicho....... nilikuwa na sababu, wao ndio wameaminishwa kwamba kuchelewa kuolewa ni janga na kwa kuwa watakuwa na nafasi finyu ya kuzaa, lakini pia wakatishwa kwamba kuzaa kabla ya ndoa ni haramu, watoto hao wataitwa haramu. kwa hiyo mwanamke anajikuta yuko kwenye wakati mgumu zaidi. anataka kuzaa japo hajapata wa kumuoa, lakini kuna sauti zinamtisha kuwa ni haramu............
hawa ndio kusudio la mada yangu.
 
Mtambuzi labda tuanzie hio sentensi yako ya mwisho.... Ni nini hasa kimetuleta hapa duniani na wajiibu wetu ni upi??

ndyoko kanisaidia kujibu.............
 
Nyerere alisema hakuna umasikini mkubwa kama umasikini wa Fikra,Mtu yeyote mwenye mawazo kama haya ni masikini wa fikra hata kama anaendesha vogue.
 


....loners die miserable BUT having someone around when you don't want them there is miserable as well!
 
Mungu ametuweka duniani tumjue, tumpende, tumtumikie, tupate kufika kwake mbinguni!!!
Hivi Mungu ni so self centred kiasi kwamba ametuumba kwa ajili ya kumpenda, kumsujudia, kuwambudu. ........................................ tu? I doubt it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…