Hata uwaeleze vipi hakuna atakayewaelewa

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,606
Reaction score
1,711
Walionena kuwa mapenzi ni ya wawili waliona mbali. Tena mbali sana. Wengi hujaribu kuomba ushauri hapa na pale, huku na kule lakini haisaidii kwa kuwa huwezi kueleza kilichojiri kati yako na mwenzako mpaka kieleweke. Ni ninyi wawili tu mnaojua nini kilitokea. Kama mmeshindwa kukitatua msitegemee eti mtamueleza mwingine aelewe. Sana sana mtaishia kuchochea umbea na majungu. Labda muende pamoja kwa mshauri nasaha. Ila hata yeye hataelewa. Atachoweza ni kuwasaidia tu muweze kueleweshana na kutatua tatizo lenu wenyewe.
 
kweli kabisa mwana...maana kwanza kabisa hawawezi kukwambia yote yaliyotokea kati yao. hivyo basi ushauri wowote ule utakaowapa haufi kwa kuwa wamekunyima wewe information muhimu ambayo ingekusaidia wewe kutoa ushauri sahihi
 
umeanza vizuri, umemalizia vibaya - hapo kwenye nyekundu kuna mgongano, sio kuwa wanakunyima ni kuwa hata wakitaka hawawezi (labda wawe wamerekodi penzi lao lote 24/7/365 + vipimo vya hisia na mawazo yao moyoni/akilini jambo ambalo nalo haliwezekani)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…