Kuna mazingira wananchi wametengenezewa na CCM kuwalazimu wao kusifia tu kusifia tu hata kama yeye na ukoo wao wote ni masikini wa kutupwa na hawana mbele wala nyuma
CCM, yenyewe imejitengenezea ulaji wa keki ya Taifa kupitia familia chache sana ambazo ndizo zitaendelea kuneemeka na mema yote ya nchi mpaka kiama, kama tu wananchi wataendelea kuwa watumwa na wajinga wa kusifia hata pasipositahili
Mtindo huu unaanza kuuona hata kwenye vyama vya upinzani! Viongozi vyama vya upinzani nao wako bize kuandaa ukoloni uleule, hawataki kuachia madaraka na kuwapa aengine, wako bize kuandalia watoto wao kukava nafasi zao na ama watu wa Karibu nao!
Tangu nimekuwa na akili, nasikia majina yale yale ya ukoo uleule iliyowahi kuwa kwenye vitengo mhimu na mpaka leo iko vilevile familia zile zile ambazo mpaka leo ndio wanakula keki ya Taifa
Majina yale yale ndiyo yanayoteuliwa kurudi kwenye ulaji ule ule na wananchi wanasifia! Hivi watanzania mmelogwa?
Unajiuliza, kwani wao wamesoma shule zipi ambazo jamii nyingine haikusoma huko?
Mitoto mingine ya hao mabwanyenye, haina hata shule, na ndiyo hiyoinayosababishia hasara nchi yetu, usimamizi mbovu na haiguswi, wanaoguswa ni wale tu ambao kwa bahati mbaya waliingia hizo nafasi licha ya ukweli kwamba, wamefanya vizuri lakini kwa kuwa sio miongoni mwa hizo familia pendwa na viongozi wa ccm wanatemwa tu
kila ukifungua mitandao ya kijamii, unakutana na Habari za walioteuliwa kushika nyadhifa, unakutana na majina yale yale ya miaka na miaka na ama watoto wa walewale waliowahi kuwa viongozi
Namna hii, unajiuliza, kwani hakuna watu wengine nao wakapewa hizo nafasi ili nao kama watanzania waile keki?
kwenye ajira za malipo mazuri bado mambo ni yale yale, mtoto wa masikini ambaye hana mtu huko, ajira za namna hiyo atazisikia tu kwenye bomba, bila kujitambua na yeye anaanza kusifia! Huo ni upumbavu kabisa!
Unasifia wenzako wanavyoishi kukwapua utajiri wa nchi yako na wewe kuishi kama mtumwa kwenye nchi yako? Ujinga