Hata Watoto Wanajua!

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,972
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 9 alikuwa anahitaji sana shilingi 100,000
(Laki moja). Akamuuliza mama yake ni jinsi gani anaweza kupata pesa hizo. Mama yake
akamwambia "muombe Mungu atakupatia. Mtoto alianza kuomba kila siku na kila
mara lakini hakupata hiyo pesa toka kwa Mungu. Hatimaye akafikia uamuzi wa
kumuandikia barua Mungu ili asome maombi yake.

Kisha akai-post barua ile. Wakati wafanyakazi wa posta wakichambua barua
kwa
ajili ya kuzipeleka sehemu husika, walishangazwa kuona bahasha iliyoandikwa
"Kwa Mwenyezi Mungu" na wakashindwa kuelewa mahali pa kuipeleka, Wakaamua
kuifungua.


Barua ilisomeka hivi:

"Mpendwa Mungu,

Jina langu ni JANET, nina umri wa miaka 9 na ninasoma darasa la tatu
katika
jiji la Dar es salaam ambalo liko katika nchi ya Tanzania , bara la Africa .


Nimeamua kukuandikia barua hii kukuomba kiasi cha shilingi laki moja baada ya
kuomba bila kupata majibu toka kwako.


Naomba sana unisaidie kwani mimi ni mtoto mdogo na sina uwezo wa kufanya
kazi na
kupata pesa. Pia wazazi wangu hawana uwezo kwani hata nchi yetu ni maskini
sana .


Natanguliza shukrani.

Wako mtiifu,


JANET."



Wafanyakazi wa posta walifurahishwa sana na barua hiyo na kisha wakaamua
waipeleke kwa Rais . Rais naye alipoipokea ilimfurahisha
sana na
kisha akamwambia Secretary wake achukue sh. 2000 amtumie mtoto huyo akidhani
kuwa pesa hizo ataziona kuwa nyingi sana .


Mtoto huyo alipopokea hizo shilingi 2000 alijibu hivi:

"Mpendwa Mungu wangu,

Nashukuru sana kwa kusikiliza maombi yangu na kunitumia pesa nilizokuomba.
Lakini nimebaini kuwa uliamua kuzituma kupitia serikali yetu ya Tanzania .
Kama
ilivyo kawaida yao hao wezi, wamekata kiasi cha sh. 98,000 kwa ajili ya
kodi ,
kwa hiyo wameniletea Sh. 2000 tu."


Kazii Kwelikweli!!!!!!!!!!!
 
Mtoto mwingine yeye alikuwa anataka baiskeli kwa muda mrefu sana ameomba kwa Mungu bila mafanikio, hatimaye akaona aibe baiskeli kwani aligundua kuwa mungu hawezi kumletea baiskeli ila anaweza kumsamehe kwa hiyo akaomba toba kwa Mungu.
 
Mfano huu alishawahi kuutoa BWM(wakati akiwa rais wa JMT),akitetea pointi yake ya kuwaponda watu wanaoilalamika serikali kwa kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…