Elections 2010 Hata wazee vijijini wanaelewa hali halisi ilivyo

PAMBANA

Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
73
Reaction score
21
Ndugu zangu hata mzee vijijini wanaelewa hali halisi na wamebadilika kutaka kuona mabadiliko katika nchi hii.Nina babu yangu mzee wa miaka 90 sasa ambaye ameona tawala zilizopita toka enzi za mkoloni na mzee huyu alikuwa ccm damudamu na usingeweza kumweleza kitu chochote kuhusu CCM.Lakini sasa amepima,kuchambua,kuchuja na kuona hali ya maisha ilivyo hasa katika kipindi hiki cha miaka mitano iliyopita anasikitika sana,amebadilika na kuwa miongoni mwa waleta mabadiliko katika nchii kabla hajafa kwa kumpigia DR.SLAA.
 
wapo wengui tuuu ndugu cha msingi tuombe sana mwenyezi Mungu amweke mtawala wa haki
 
Mambo yamebadilika mkuu!!! Kila mtu anataka changes!! Wasiotaka changes ni wale tu wanaofaidika na utawala huu uliooza!!!:doh:
 

Mimi baba yangu mzazi ambaye yuko kwenye mid seventies na ni CCM damu lakini naye anaongelea mabadiliko. Nadhani hii ni changamoto hasa kwa vijana wa leo ambao mabadiliko ya kweli yatakuwa na manufaa zaidi kwao kuliko sisi wazee ambao muda wetu wa kuwepo hapa duniani ndio unayoyoma.
 
Jamani naamini kuna watu wamekufa kwa kukosa huduma mbalimbali amabayo serikali ingetakiwa kutoa mfano wajawazito. Hii damu na vilio ni sala tosha kwa changes.

Lets continue praying for our beloved nation. against mafisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…