hataki mpangaji mwenye gari

Jamani MadameX na Preta wengine wana magari hawana nyumba kwa kuwa ni ya bahati nasibu lakini pia huyo baba mwenye nyumba nae ana roho ya kwanini, ndo mpaka lift hataki nadhani huo ni uzuzu na hatokuja kununua gari kwa style hii.
 
Last edited by a moderator:
Hapa naona kuna hoja moja tete.

Kwanza, wenye nyumba nji hii wamekuwa kama Miungu watu...kuna watu wanadhani ukishajenga nyumba, ukamweka mpangajim ni kama 'mjakazi' wako...wanasahau kuwa mtu akishalipa kodi mkataba ni kuwa yeye ana nyumba anaitumia, wewe unatumia pesa zake? itakuwaje mpangaji akimwambia mwenye nyumba pesa alizompa asinywee bia? au asihonge nyumba ndogo?
Ni utamaduni ambao haujabalansi niseme....

Inabidi tufike mahali tujue na kujiuliza itakuwaje kila mtu akajenga nyumba.....kingine wenye nyumba tunachosahau ni kuwa mtu anapanga kwa sababu mbali mbali na sio kwamba yeye hana nyumba anayomiliki! Imagine wale wanaohama kikazi kutoka mji mmoja hadi mwingine..atajenga nyumba ngapi?

Kwa hili huyo mzee ni kilaza, ana kijiba cha roho na mbumbumbu wa maisha, Kuwa na gari siku hizi imekuwa kama basic need hasa kwa maeneo ya mijini kusiko na usafiri wa uhakika wa public. sasa huwezi kunipangisha nyumba then unambie nisiwe na gari kisa tu wewe huna?

Kuna mmoja anasema ni kuwatia wivu wa maendeleo sijui nini...kama ni hivyo basi mwenye nyumba naye angenunua gari yake ili akamilishe 'maendeleo'...maendeleo ni nini kwani hasa?
 

Project ya nyumba nayo ngumu maana msingi tu unaweza kukulamba 4 million bado kunyanyua ukija roofing utalamba kati ya 5 million - 10 milion depending na aina ya bati, milango, madirisha, rangi, makaro ya maji machafu na uzio, hapo si itafika zaidi ya milioni 50 kabisa wakati gari unaweza pata la mpaka 4 million na kuendelea
 
huyo baba mwenye nyumba ana wivu tu....

Hivi kila mtu akijenga nani atakuwa mpangaji.....

Ila mie ningekuwa ni mpangajiwake walllhahiiiiiiii yaani gari yangu, kodi nimoe, nichangie buku buku za paking na ulinzi, visa anifanyie then nimpe lifti? Thubutuuuu atakuwa anaiona ikipaki tu....
 
Jamani MadameX na Preta wengine wana magari hawana nyumba kwa kuwa ni ya bahati nasibu lakini pia huyo baba mwenye nyumba nae ana roho ya kwanini, ndo mpaka lift hataki nadhani huo ni uzuzu na hatokuja kununua gari kwa style hii.

Sasa wote wamepata kwa bahati nasibu, basi kama mtu anaakili si unauza gari angalau ununue kiwanja.
 

safi sana, wenye nyumba wengine viazi sana....
 
hivi jamani.....gari ni shs ngapi na nyumba shs ngapi.....?

Nyumba si inaweza kuwa kati ya 30m - 60m kulingana na mahitaji yako na gari lipo la kuanzia 2m - 200m kulingana na uwezo wako
 

nimekupenda bila hela shemeji.......
 
utanunuaje gari nyumba ya kupanga......?

Hiyo hai-justify mateso ya mwenye nyumba.
Wengine tumejenga tayari, ila tumehamishwa kikazi hadi mikoani, sasa mnataka uwe tunajenga kila mahali tunakohamishiwa?
 
Hiyo hai-justify mateso ya mwenye nyumba.
Wengine tumejenga tayari, ila tumehamishwa kikazi hadi mikoani, sasa mnataka uwe tunajenga kila mahali tunakohamishiwa?

Exactly one of my points mkuu Idimi....watu wanashangaza sana aisee...
 
Last edited by a moderator:
Jaman maisha ya dar es salaam bila gari ni tabu as kwenye proffessional nyingine smartness ni muhimu sana, kwa usafiri wa daladala unaweza kwenda kwenye meeting na shati chafu tena na clients ukaonekana kituko, gari hadi million 7 to 10 unapata, but kiwanja gan itapata kwa bei hiyo harakaharaka, huyo mwenye nyumba ana matatizo ya akili but gari sio luxury need ni essential ndo maana tumenunua mapema, but kujenga needs some times, I plan to build my house around 5-7 years pole pole sasa mda huo wote nikakae wapi kama nisipopoanga.
Also nina imani kujenga sio kazi, kazi ni kupata kiwanja kizuri kwenye location unayopendelea kuishi.

Jaman magari sio utajiri,
 
Mimi nina gari na nyumba na hata mashamba.Lakini ushauri huu ni wa bure kwa vijana.Si busara kununua gari wakati huna hata kibanda.Nunua kiwanja halafu anza hata na vyumba viwili.You look sensible.
 


hapo sasa da preta! btw ulibadli avatar siku za karibuni ..?!

ndio dr.....lakini nilijishtukia....nikarudisha ya zamani.....hujambo lakini....?
 
Samahani dada Preta, wewe ni mchaga?

Kaka zenu nasikia ndo huwa hawaoi kabla hawajajenga kwao na mjini, ni kweli?

hahaha Bigirita chezeya kulala gheto moja na mdingi? laana hiyo!!!! Yaani unanyooka hapa, dingi naye ananyooka chumba jirani? laana na nusu yake!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…