Huu ni ujinga wa kiwango cha PhD na hili limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa wasanii na wanamichezo wanaotoka katika dunia ya 3 haswa haswa Africa na America ya kusini wanapofanikiwa na kuwa katika vilele vya nafanikio yaliyotokana na nguvu na jasho lao.
wamekuwa wakifanya mambo ya hovyo kabisa bila kufahamu athari zake baadae kutokana na kuwa na elimu ndogo,ufahamu mdogo wa jinsi mambo yanavyotakiwa kwenda baada ya kufanikiwa, na kuzungukwa na magenge ya mafisi wanaotamani kile walichonacho na sio muhusika tumeona wasanii wengi sana na wanamichezo wengi sana wanaoishi maisha ya shida sana na dhiki kubwa mno kama vile hawakuwahi kufanikiwa kwenye maisha yao lakini ukichunguza kwa umakini untagundua walipokuwa mastar wakubwa hawakuwaza wala kufikiri kuwa kuna maisha baada ya vipawa vyao kufika ukomo badala yake wakawekeza katika ujinga na upumbavu wakalewa sifa kutembea na misafara mikubwa na walinzi wengi wanaowahgarimu pesa nyingi sana bila sababu ya msingi faida wanazopata ni sifa tu na ufahari usiokuwa na msingi.mimi na wewe Nafikiri tunawafahamu matajiri wengi sana wakubwa na wenye pesa nyingi sana kuliko hao wasanii na wanamichezo lakini hatujawahi kuwaona wakifanya mambo ya hovyo na ya kijinga kama haya hawana misururu ya watu kila wanapokwenda na wala hawatembei na walinzi wengi hivyo kama viongozi wa kisiasa, sasa tujiulize mimi na wewe ni nani atakaefikiria kumteka mtu kama Harmonize na wengine wanaofanya hivyo aache kufikiria kumteka tajiri kama Mo Dewji,Bakharesa au ailko dangote ndio maana tunashauriwa ukiwa na kipaji/talanta kichanganye na elimu ili kuepuka kufanya mambo ya hovyo kama haya badala ya kuwekeza kwenye biashara wanawekeza kwenye ujinga na upumbavu,
#Kweli watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifaπ³π³π³π³π³πββοΈπββοΈπββοΈπββοΈπββοΈπββοΈπββοΈ
C&P
View attachment 1211489