Hatari mazoezi ya kukimbia(jogging)

Ni vyema kufanya mazoezi kwenye less traffic road..... Hizi barabara busy huwa zinachangamoto sana.

Kuhusu why not viwanjani?

Kwa uzoefu wangu kufanya mazoezi uwanjani ya kukimbia huwa una cover less distance kuliko kukimbia barabara za Lami.
Ili kupata km 1 kwa uwanja wa 100 kwa 50 itakubidi uzunguke mara 3 na nusu uwanja.... Sasa kupata km 10 tu itakubidi uzunguke uwanja mara 35..... Hii inatia uvivu....

Ila barabarani unaenda tu na kupata 10km ni easy pia kuna elevation zinasaidia.
 
Kichwa kiwe "HATARI ZA MAZOEZI YA KUKIMBIA PEMBEZONI MWA BARABARA"
.... hao ndio waandishi wetu chief. Binafsi nikajua kuna utafiti umethibitisha jogging ni hatari kwa afya kumbe tofauti kabisa; anamaanisha mazingira ya jogging mijini Tz sio salama hususan pembezoni mwa barabara. Elimu yetu ni shida sana.
 
Nimekutana na watu wakifanya mazoezi ya kukimbia pembezoni mwa bara bara hizi ni athari;
1.Kugongwa na gari
2.Kuvuta moshi utokanao na magari
NOTE: Kwanini viwanja vya michezo visitumike?
Kila kitu maishani ni risk tu
 
Kuna kipindi nilikuwa napenda kuimbia barabarani uswahilini mida ya asubuhi. Mambo yalikuwa safi. Baada ya miaka kadhaa niliporudia kukimbia barabara hiyo nikakuta ujenzi umesogea sana barabarani. Halafu majibwa koko kibao. Nikasitisha zoezi.

Kuna hatari nyingi kukimbia barabarani
 
Run for your life...πŸƒπŸ½β€β™‚οΈπŸƒπŸ½β€β™‚οΈπŸƒπŸ½β€β™‚οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈπŸƒπŸ½β€β™€οΈ
 
Mkuu ni hatari kukimbia kama umezidi 45years (tetesi)
 
Nimekutana na watu wakifanya mazoezi ya kukimbia pembezoni mwa bara bara hizi ni athari;
1.Kugongwa na gari
2.Kuvuta moshi utokanao na magari
NOTE: Kwanini viwanja vya michezo visitumike?
Tunaomba Takwimu

Ni wakimbiaji wangapi wamekanyagwa na magari makubwa kwa mwaka jana?

Vipi kuhusu faida za jogging ukilingamisha na ubebeji wa mavyuma mazito?
 
Nimekutana na watu wakifanya mazoezi ya kukimbia pembezoni mwa bara bara hizi ni athari;
1.Kugongwa na gari
2.Kuvuta moshi utokanao na magari
NOTE: Kwanini viwanja vya michezo visitumike?
Ni kweli kufanya mazoezi barabarani ni hatari, lkn kutokufanya mazoezi ni hatari zaidi.

Muhimu tu ni kuchukua kila tahadhari iwapo unakimbia barabarani; mfano;
1. Unapokimbia always tumia upande wa kulia (yaani kimbilia na kutazama magari yanayokuja mbele yako).

2. Kama unakimbia jioni au asbh kukiwa hakujapambazuka vzr, kuwa na reflectors Miguuni na mkononi na jitahidi kuvaa nguo zinazoo ekana kirahisi ili uonekane kirahisi na watumiaji wengine wa barabara.

3. Jitahidi ikibidi mkimbie zaidi ya mtu mmoja ili ikitokea dharura mmoja aweze kumsadia mwingine hasa mnapokimbia long run Km 21.1 na kuendelea hasa kwa pace chini ya 5.20M/Km maana inafika mahala mwili na akili vinachoka.

Kwangu mm mambo haya yamenisaidia sana na ninazidi kukuwa kila siku kimazoezi na kwa sasa i do 200km running challenge kila mwezi na ninamudu. Niwatie Moyo tuendelee na Mazoezi, Jogging haidanganyi yaani ukifanya kwa nia in very short of time matokeo yanaonekana.
Msingi kula kwa afya, punguza vyakula vya wanga, uepuke mlo wa usiku, ukishindwa punguza vzr zaidi ukila Matunda pekee.
hii ni running challenge yangu ya June, 2021 ambayo nimekamilisha leo na hii ni kila mwezi πŸ‘‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…