Ni kweli kufanya mazoezi barabarani ni hatari, lkn kutokufanya mazoezi ni hatari zaidi.
Muhimu tu ni kuchukua kila tahadhari iwapo unakimbia barabarani; mfano;
1. Unapokimbia always tumia upande wa kulia (yaani kimbilia na kutazama magari yanayokuja mbele yako).
2. Kama unakimbia jioni au asbh kukiwa hakujapambazuka vzr, kuwa na reflectors Miguuni na mkononi na jitahidi kuvaa nguo zinazoo ekana kirahisi ili uonekane kirahisi na watumiaji wengine wa barabara.
3. Jitahidi ikibidi mkimbie zaidi ya mtu mmoja ili ikitokea dharura mmoja aweze kumsadia mwingine hasa mnapokimbia long run Km 21.1 na kuendelea hasa kwa pace chini ya 5.20M/Km maana inafika mahala mwili na akili vinachoka.
Kwangu mm mambo haya yamenisaidia sana na ninazidi kukuwa kila siku kimazoezi na kwa sasa i do 200km running challenge kila mwezi na ninamudu. Niwatie Moyo tuendelee na Mazoezi, Jogging haidanganyi yaani ukifanya kwa nia in very short of time matokeo yanaonekana.
Msingi kula kwa afya, punguza vyakula vya wanga, uepuke mlo wa usiku, ukishindwa punguza vzr zaidi ukila Matunda pekee.
hii ni running challenge yangu ya June, 2021 ambayo nimekamilisha leo na hii ni kila mwezi [emoji116]
View attachment 1833979