Hatari redio za simu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo.
Akizungumza na gazeti la Amani mapema wiki hii jijini Dar es Salaam, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’.
“Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka.

Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo.
Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya saa nne. :A S thumbs_down:

















 
naona kama dr amekurupuka.Mi nilitegemea anatoa matokeo ya utafiti!.Hiyo statement ni tooooo general.
 
Mimı bıla headphone sıjuı kama sıku ınaweza kuısha,cha msıngı nı kumwomba MUNGU atuepushıe na hayo madhara,
NB:too much of anythıng ıs hamrful.
 
ccm yenyewe ni zaidi ya saratani.
serkali yake ni zaidi ya ukimwi,sasa kwa nini tuogopo viredio vya simu?
huo utafiti wako peleka kwenye maisha bora si tanzania.huku tunauwawa na vingi tena vya kutengenezewa na tuliowaamini.
acha tujifariji kwa bongo fleva labda tutasahau shida zetu.
 
<br />
<br />
we kila kitu unawazia siasa hata mkeo ukimfumania utadai katumwa na CCM
 
utafiti unasema radio na mionzi ya radio sasa speaker na ngoma ya sikio it has nothing to do with radiotion.

Maelezo ya dr. Ni incomplete and not focused katika subject matter
 
Kila kitu kina madhara kama utatumia kuzidi i.e. too much of anything is harmful. Nadhani madhara ya headphones ni madogo kuliko alivyo exaggerate huyo DR. Vp kuhusu watu wanaotumia headphones mda mrefu kama pilots, phone operators n.k. Acha tupunguze stress hususan kwenye foleni au kipindi hiki cha mgao.
 
Nachojua WHO wametoa report kuwa mihonzi ya simu za mkononi inaleta kansa ya uvimbe kichwani. Na hii ni utafiti ulofanywa na jopo la wataalamu wa kimarekani walio kuwa commissioned na WHO. Hivyo ni safe kutuma sms than talking to phones fo long time. Hii imekuwa ni news kwa nchi nyingi zilizoendelea recently nashangaa Tz wanahabari hawaja wahabarisha watu au voda na tigo na wengine wame tip kubana hiyo habari. Huo utafiti umesema risk kwa watoto wadogo ni kubwa zaidi kwa kuwa fuvu lao ni rahini. Wamesema mihonzi ya simu ni sawa na effect ya dawa kama DTT (sijuhi nimepatia ile dawa ya wadudu) na ni almost ina nguvu kama mihonzi ya microwave. Kwa hiyo wandugu technolojia zitatuua, bora simu zetu za zamani za TTCL.
 
Phone operators wanalalamika sana masikio yameharibika. Kuna dada alikuwa anafanya kazi Zain customer care. Alinisimulia kuwa muda wote anatumia headphones kujibu wateja kwa sasa masikio yake yameharibika na ameacha kazi . Na alinambia si yeye tu watu wengi wanabwaga manyanga. Hata wewe jaribu kukaa na headphones the whole day uone tofauti ya uwezo wako wa kusiki.
 
daa, nmepata kitu hapa, na vp kma una2mia sana sim, kwa kwa kuchart kwa sms, internent. Maana m hapo 2 ndo nimewezwa. Na betri 3. Kwa kaz maja 2, nayo n kuchart. Aaah si ndo tunapunguza stress jaman?...ewaaaa 2shauriane jaman ati docta!
 

...asante' DR.

Simu yako ni HATARI SANA
kwenye Afya yako.
Fahamu MADHARA yatokanayo na
simu yako na JINSI YA
KUYAPUNGUZA.
Simu tunazozitumia hutoa mionzi
(radiations) hatari sana ijulikanayo
kama "Electromagnetic waves"
wakati wa kupiga/kupokea simu,
kuperuzi Internet, nk..
Madhara ya Mionzi hii;
1. Husababisha Saratani ya Ubongo
(Brain Cancer) na ngozi (Skin
Cancer).
2. Husababisha hitilafu kwenye
Ubongo na hii hupelekea kupoteza
kumbukumbu, uwezo mdogo wa
kupambanua mambo na umakini
(Concentration).
3. Husababisha upungufu wa
mbegu za kiume na hata utasa
(Impotence) kwa wanaume.
4. Huongeza shinikizo la damu.
Jinsi ya kupunguza Athari
zitokanazo na Mionzi hii hatari;
1. Weka vifaa maalum vya
kupunguza mionzi (Radiation
absorbers) kwenye simu yako.
Vinapatikana madukani.
2. Usipende kuweka simu mfukoni
endapo huitumii. Wakati wa kulala
weka mbali angalao SM 30 kutoka
ulipo.
3. Simu iwapo mfukoni, upande wa
Vitufe na kioo cha simu ndio
kielekee mwili wako!
4. Tumia "headsets" au "Kipaza
sauti (Loud Speaker). Hii
hukusaidia kuwa mbali na mionzi
wakati wa kupiga/kupokea simu.
5. Usiitumie simu yako iwapo ina
"bar" moja au mbili za
"network" (Low Network Signal).
Wakati huu simu inafanya kazi
kupita kiwango cha kawaida hivyo
huongeza wingi wa mionzi.
6. Wakati wa kupiga simu, subiri
ipokelewe ndio uisogeze karibu ya
mwili (mf. Masikioni).
7. Iwezekanapo, penda kuwasiliana
kwa ujumbe wa sauti (text msg)
kulipo kupiga simu.
Simu ni muhimu sana katika
Maisha yetu ya sasa.
Hutuunganisha na ulimwengu
uliogubikwa na Maendeleo ya
Sayansi na Teknolojia.
Sanjari na hili, tunapaswa kuwa
makini katika juhudi za kujaribu
kuepuka Madhara yatokanayo na
simu kama ilivyoainishwa hapo
juu.
 
Tuliofanya kazi za customer care tupo hatarini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…