Hatari ya unene

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363



HATARI YA UNENE:

MOJA ya hatari inayowakabili watu duniani ni unene (au kuwa na kitambi au kuwa na uzito mkubwa). Janga hili linawakabili wakubwa kwa watoto.

Unene, kitambi au uzito mkubwa ni mambo ambayo yana athari mbaya kwa afya. Hata hivyo, watu wengi wenye hali hiyo hawaoni hatari inayowakabili. Kibaya zaidi kuna baadhi ya watu huona ufahari kuwa wanene au kuwa na kitambi. Yaani huona kuwa vitu hivyo huonyesha hali nzuri ya maisha. Kwa mfano, baadhi ya watu hukiita kitambi Economic Curve.

Kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo hili na hali ya jamii yetu, makala ya wiki hii inatazama sababu zinazoleta tatizo hili, hatari ya janga hili na namna ya kulikabili.

Unene au uzito mkubwa hali zote hizi tatu kwa Kiingereza hujulikana kama Obesity. Vile vile, mtu akiwa na moja ya hali hizo hujulikana kuwa ana Obesity.

Unene au kitambi au uzito mkubwa tunaweza kusema kama ni ile hali ambayo mwili huwa na kiasi kikubwa cha mafuta kuliko ilivyokawaida.

Kutokana katika vyakula, mwili unapata mafuta kwa njia kubwa mbili. Kwanza ni pale mtu anapokula vyakula vyenye mafuta. Pili ni pale mtu anapokula vyakula vyenye wanga au sukari.

Kwa kawaida vyakula vyenye wanga au sukari (mfano mahindi, mchele, asali, ngano, sukari na kadhalika) hutumika kuupa mwili nguvu. Ziada ya vyakula hivi mwilini huhifadhiwa kama Glycogen.

Kwa baadhi ya watu, ziada ya chakula mwilini huwa kubwa. Kwa hiyo kiasi fulani ya ziada hiyo huhifadhiwa kama Glycogen kama nilivyotangulia kusema, na ziada nyingine hubadilishwa na kuwa mafuta ambayo huhifadhiwa katika viungo mbalimbali mwilini. Mafuta haya ndiyo yanayoleta unene, kitambi au uzito mkuwa.

Mpaka hapa tumeona kuwa moja ya sababu ya unene, kitambi au uzito mkubwa ni aina ya kiasi ya chakula anachokula mtu. Hata hivyo kuna sababu nyingine zinazochangia janga hilo (unene, kitambi au uzito mkubwa).

Moja katika kundi la sababu nyingine ni maumbile (Genetic). Wataalamu waliofanya utafiti juu ya suala hili wanatuambia kuwa kama baba na mama wote ni wanene, kuna uwezekano wa asilimia themanini (80%) wa kuzaa watoto wanene.

Watafiti wanaendelea kusema kuwa kama mmoja kati ya wazazi hao ni mwembaba, uwezekano wa kuzaa mtoto mnene unapungua na kuwa asilimia arobaini (40%) badala ya ile thamanini.

Zaidi ya sababu hizo, ukosefu wa mazoezi ya viungo nayo ni sababu kubwa inayowafanya watu kuwa wanene au kuwa na vitambi au kuwa na uzito mkubwa.

Kutazama televisheni (TV) kwa muda mrefu pia ni sababu nyingine inayoleta Obesity kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni. Kutazama TV kwa muda mrefu kunaleta ugoigoi (Inactivity) na hatimaye mafuta mengi mwilini.

Baadhi ya watu wanene au wenye vitambi au wale wenye uzito mkubwa hawaoni kama wana dosari yoyote. Na inafikia mahali wanahoji kwa nini wapunguze uzito au unene?

Mtazamo wa watu hawa siyo sahihi kwa sababu, unene, kitambi au uzito mkubwa ni mambo ambayo yana athari mbaya kiafya kama ninavyoeleza hapa chini.

Watu wanene (wenye vitambi, uzito mkubwa) wako katika hatari kubwa ya kupata magonjwa kama vile ya moyo, strok (brain strokes), ini, figo, kibofu cha mkojo, saratani (cancer) na kadhalika.

Vile vile watu wa kundi hili huwa dhaifu (wazito) wakilinganishwa na watu wembamba. Katika hali ya hatari (kama vile moto, ajali, wanyama wakali na kadhalika) watu wanene huwa na wakati mgumu kujiokoa.

Baada ya maelezo ya hapo juu ni vyema sasa tuimalizie makala hii kwa kutazama njia bora za kupunguza kama siyo kuondoa kabisa tatizo tulilolijadili.

Kwanza, watu walioathirika (wanene, wenye vitambi au wenye uzito mkuwa) na wale ambao hawajaathirika wafuate kanuni bora za chakula na lishe, na hasa mlo kamili (balanced diet). Makala zetu za nyuma zilijadili kwa kina dhana ya mlo kamili.

Hata hivyo, tunawashauri wananchi wakutane ana kwa ana na wataalam wa lishe au wafike katika vituo vya afya kwa msaada zaidi.

Pili, watu wawe na utamaduni wa kufanya mazoezi ya viungo. Pia kazi za mikono kama vile kulima, kutwanga, kufua nguo, kuendesha baiskeli, kubeba mizigo, kutembea kwa mguu kwa umbali fulani na kadhalika zinaweza kusaidia kupunguza mafuta mwilini.

Tusibweteke na teknolojia ya kisasa kama vile magari. Sambamba na hilo, ibada ya kufunga swaumu nayo inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mafuta mwilini. Kwa mfano, Waislamu wanafunga nyingi za sunnah mbali na ile ya lazima (Ramadhani).

Moja ya funga za sunnah ni ile ya kufunga siku moja na unafungua siku ya pili (sunnah ya Nabii Daudi a.s.) na unaendelea kwa hivyo hivyo. Au sunnah ile ya kufunga Jumatatu na Alhamisi ya kila wiki.

Tatu, ni vyema mtu mnene akaoana na mtu mwembamba. Kwa maneno mengine, si vizuri watu wanene wakaoana, labda iwe hakuna budi.

KWA MTU MWENYE UNEN AU KITAMBI AU TUMBO KUBWA NA MAFUTA ANATAKA KUPUNGUWA

DAWA NINAYO TEMBELEA HAPA BONYEZA
Topic: Good news kwa wale wenye kutaka kupunguza uzito wa mwili na unene na mafuta mwilini
 
asante sanaaaaa! wengine ni kweli kabisa genetical.swali langu ni moja je kwa mfano mtu anataka apungue tumbo tu je hii dawa inamfaa?
 
asante sanaaaaa! wengine ni kweli kabisa genetical.swali langu ni moja je kwa mfano mtu anataka apungue tumbo tu je hii dawa inamfaa?
Ndio mkuu Dawa yangu itakufaa kupunguwa tumbo .
chupa 6 Bei yake ni Dola330 pamoja na gharama za utumaji Dawa . Ukizihitaji hizo dawa jaribu kunitumia mail kwa njia ya-




barua ya Pepe Email yangu ni hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 

Attachments

  • FITOFORM PLUS.jpg
    42.4 KB · Views: 90
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…