Dr Riwa yupo najua atakuja kusaidia hili.
Laura unanitafutia kesi hivooo...mie sina jibu la kila swali au usahuri kwa kila tatizo. Ila kwa kuchangia ni kuwa....mara nyingi 'ububu' husababishwa na kutosikia. Mtoto akiwa kiziwi, hajawahi kusikia sauti yeyote, basi hawezi kusema zaidi ya ile bee beee bee na kutoa ishara.
Natumai mpaka mwanao anafika miaka mi3 utajua tu kama anasikia au la, mwanao anasikia? kama anasikia basi si bubu, ana tatizo jingine tuu.
Maswali machache kabla sijachangia zaidi...
- Je, mwanao alilia mara tu baada ya kuzaliwa? au walimgeuza geuza na kumpiga piga na kumpitisha mpira puani ndio akalia? alilazwa kwa siku kadhaa hospitalini baada ya kuzaliwa akihitaji msaada wa mashine ya kupumulia?
Kwa sababu mtoto anapochelewa kulia baada ya kuzaliwa, basi anachelewa kupumua mwenyewe na hivyo kuchelewa kupata damu yenye oxygen ya kutosha kwenye ubongo na kuathirika. Athari hizi za ubongo huchelewesha makuzi yake kiakili na wakati mwingine hata kimwili.
- Je, mtoto wako amechelewa katika makuzi, mfano alichelewa kukaza shingo? alichelewa kukaa, kutambaa, kusimama, kutembea n.k?
Kama ni hivyo kuna uwezekano mkubwa alipata athari nilizosema hapo juu.
- Je, mtoto wako hana matatizo ya ulimi mfano ulimi mkubwa, au umevimba na kujaa mdomoni? Je ana kinyama kimeshikilia ulimi ukikagua chini ya ulimi (Tongue tie)?
Tongue tie ni vigumu kunotice kama mama hamuwa makini, kanashikilia ulimi kwa chini basi mtoto anachelewa kuongea, huwa kinakatwa kwa operation hospitali..
Nijibu niendelee..