Hati mikili za Ardhi 310 zatolewa Jijini Mwanza, Waziri Ndejembi awafikia na kusikiliza wananchi

Hati mikili za Ardhi 310 zatolewa Jijini Mwanza, Waziri Ndejembi awafikia na kusikiliza wananchi

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amewahisi wananchi waliopokea hati miliki za maeneo yao kuzitunza kwa kuwa ardhi ni mtaji waitunzi ili iwatunze.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa kauli hiyo jijini Mwanza wakati wa Kliniki ya Ardhi inayofanyika jijini humo kwa siku mbili kuanzia Oktoba 12-13, 2024 ambapo jumla ya hati miliki za ardhi 310 aimetolwa.

“Lengo la ziara yangu hapa mkoani Mwanza ni kuwafikia wananchi na kusikiliza changamoto zao zinazowakabili katika sekta ya Ardhi na kuhakikisha wananchi wetu na wakazi wa Jiji la Mwanza na mkoa huu wanapata haki kwenye ardhi yao kwa kumiliki maeneo yao kwa kuzingatia nyaraka walizonazo” amesema Waziri Ndejembi.

Akiongea na wananchi kwenye viwanja vya Jiji la Mwanza, Waziri Ndejembi amewasihi wananchi hao kuwa masuala yote ambayo yapo kwenye muhili wa Mahama waende kutafuta haki zao ili kutoingilia muhimili mwingine kiutendaji na kusisitiza masuala yote ambayo hayana mwingiliano yatatatuliwa kwenye Kliniki hiyo.

“Changamoto niliyoiona hapa, mengi ni ya kisheria zaidi ambapo katika utekelezaji unakuta kuna katazo la Mahakama, lakini mwananchi anawasilisha malalamiko kwenye Kliniki ya Ardhi haelezi kwa undani nini kinaendelea katika eneo husika, unapoenda kwenye utekelezaji mihimili haiwezi kuingiliana kiutendaji kwa kuwa inaheshimu mamlaka ya mhimili mwingine” Amsema Waziri Ndejembi.

Soma Pia:
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Bw. Kibamba Kiburwa amesema jiji hilo linafanya kazi kuhakikisha wananchi wanapata haki zao za ardhi ili waendelee na kazi za kimaendelo.

Kwa upande wao wananchi Grace Sukali mkazi wa Nyahingi Nyamagana na Julieth Mungo mkazi wa Malya Kwimba mkoa wa Mwanza wamesema walipigiwa simu kuja kukabidhiwa na kuchukua hati za viwanja vyao na Waziri mwenye dhamana ya ardhi na kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka wana Mwanza huku

Mzee Mathias Lung’wesha mkazi wa Bulyankhulu Ilemela Mwanza, kwa sasa anaishi mkoa wa Morogoro anasema umefika wakati sasa hati miliki za kidigitali zitolewe nchi nzima ili kuondoa mkanganyiko ambao unaweza kusababishwa kwa mfumo wa hati ambao bado unatumika maeneo mengi nchini.
 
Mbona Dar es Salaam Hati hazitolewi?
Manispaa ya Ubungo hadi Hati kupatikana ni machozi jasho na damu.
 
Back
Top Bottom