Jamani naombeni niulize.ili mnisaidie nifahamu. Ni mara nyingi sana nasikia kwamba kama unataka mikopo ya benki kwa madhumuni mbalimbali utasikia uwe na hati ya kiwanja au hati ya nyumba. Kile nisichokifahamu ni hiyo hati ya kiwanja/nyumba. Hivi hati hiyo hasa ni kitu gani, na inapatikana vipi? Au ndo ile fomu mnayoandikiana na mtendaji wa kijiji/kata mbele ya mashahidi pale mtu anaponunua/kuuza kiwanja? Kweli sifahamu naombeni mnifahamishe