Hati ya kiwanja/nyumba

Adm

Senior Member
Joined
Sep 19, 2010
Posts
149
Reaction score
45
Jamani naombeni niulize.ili mnisaidie nifahamu. Ni mara nyingi sana nasikia kwamba kama unataka mikopo ya benki kwa madhumuni mbalimbali utasikia uwe na hati ya kiwanja au hati ya nyumba. Kile nisichokifahamu ni hiyo hati ya kiwanja/nyumba. Hivi hati hiyo hasa ni kitu gani, na inapatikana vipi? Au ndo ile fomu mnayoandikiana na mtendaji wa kijiji/kata mbele ya mashahidi pale mtu anaponunua/kuuza kiwanja? Kweli sifahamu naombeni mnifahamishe
 

hiyo unayoandikishiana na muuzaji inaitwa hati ya mauziano. hakuna kitu kinachoitwa hati ya nyumba. Nahisi unamaanisha hati ya kiwanja. if yes hiyo hutolewa na kamishna wa ardhi. pia zipo leseni za makazi kwa maeneno yasiyopimwa zinazotolewa na halamshauri hasa za dar es salaam.

benki huwa wanapokea hati zote zilizotajwa hapo juu ingawa benki zile kubwa hawapokei leseni za makazi wala hati za mauziano kwa ajili ya mikopo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…