sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 649
Hati ya mashtaka ndiyo inayoanzisha rasmi mashtaka dhidi ya mshtakiwa yeyote wa makosa ya jinai.Hati hiyo hutayarishwa kwa msingi wa kisheria ambapo lazima izingatie masharti kadhaaa muhimu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sharti moja muhimu katika uandishi wa hati ya mashtaka au taarifa ya mashtaka ni kuwa kwanza lazima itaje kosa na maelezo ya kosa analotuhumiwa kulitenda mshtakiwa. Hii ni kwa mujibu wa matakwa ya kifungu cha 132 cha SHERIA YA MWENENDO WA MASHTAKA YA JINAI YA MWAKA 1985 [Sura ya 20 ya Mapitio ya 2002] maarufu "CPA". Mfano, kama kosa ni la wizi maelezo ya hati ya mashtaka yataeleza hivyo na kifungu husika cha sheria.
Wakati mwingine katika hati ya mashtaka kunakuwa na maelezo ya kosa fulani kwa kifungu fulani cha sheria na adhabu yake kutolewa na kifungu kingine cha sheria. Mfano ni wizi ambao hufafanuliwa katika kifungu cha 258 ambapo adhabu huelezwa katika kifungu cha 265 cha SHERIA YA KANUNI YA ADHABU, SURA 16. Hivyo ni makosa kwa hati ya wizi kutoa maelezo ya kosa kwa mujibu wa kifungu cha 258 badala ya kifungu cha 265.