Nakumbuka mpango ule walianza na vijiji vya mfano vichache kwa kila Wilaya, na utakuta Wilaya nyingine wameshakamilisha ktk vijiji vichache na wilaya nyingine bado. Kuna kijiji niliandikisha jina mwaka mmoja umeshapita,hakuna hata mmoja pale kijijini aliyepata hiyo hati. Cha ajabu kijiji cha jirani wilaya nyingine mkoa huo huo unaweza kupata ndani ya miezi mitatu hivi. Kuna wilaya nyingine huko mkoani Njombe, mtalaam wa ardhi alikwenda kupiga kambi kijijini kwa ajili ya hati, lakini wilaya ya jirani mtalaam hana habari.
Kwa ufupi, haieleweki. Huku pwani sijasikia kijiji cho chote. Labda Magamba wakiamua.