Hati za mashamba~Bagamoyo

KORBOTO

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2014
Posts
1,848
Reaction score
2,446
Habar za jumapili wanajukwaa, happy valentine day to you ALL.
Naombeni kujua kuhusu mada husika hapo juu, wengi tumekuwa tunanunua mashamba wilaya ya bagamoyo na wilaya za jirani na dar, ningependa kujua kama kuna utaratibu wa kuweza kupata hati ya kumiliki shamba langu. Hati itakayonisaidia kupata mkopo wa kutosha tu bank yoyote hapa dar.
Mfano shamba la ekari 5 maeneo ya kiwangwa naweza kupata mpaka mkopo wa bei gani? Shamba la ekari 20 maeneo ya Bwawani (mpaka na moro) naweza kupata mpaka mkopo wa bei gani?

Kama unainformation au experience yoyote kuhusiana na haya mambo tafadhali saidia, do not limit urself kwenye hayo hapo juu tu.
Natanguliza shukrani
 
Mimi nafahamu watu ambao wanaweza kukusaidia kupata hati.Nijulishe iwapo unahitaji contact zao.
 

KORBOTO kwanza hongera sana kwa kununua mashamba, hilo ni jambo jema sana kwa future yako na familia yako. ....

Kuhusu kupata mkopo kutoka bank yoyote kwa kuweka collateral ya mashamba uliyonayo. ...tatizo kubwa liko kwenye urasimu wa serikali hii. ..maana ili mashamba yako yakubalike kama dhamana ni lazima yawe na hati, ama hakimiliki ya kimila au hati ya shamba kwa maana ya title deed. ..

Process za kupata hakimiliki ya kimila ni kwamba ni lazima kijiji kiwe kimepimwa na kupatiwa cheti cha ardhi ya kijiji, hiki ni tofauti na cheti cha usajili wa kijiji.

Na ili kijiji kipimwe mipaka yake ya ardhi na kisha kupewa cheti cha ardhi ya kijiji, ni lazima kijiji husika kiunde kamati ya matumizi bora ya ardhi ambayo itakuwa kushirikiana na kamati ya matumizi bora ya ardhi ya wilaya kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji. ...

Kingine kijiji lazima kijenge masijala ya ardhi ya kijiji. ...Baada ya hayo kukamilika ndipo unaweza sasa kuomba kupimiwa shamba lako na kisha kupewa hakimiliki ya kimila ambayo ina nguvu ya kisheria kukuwezesha kuitumia kama live capital kwa kuiweka dhamana benki ili upate mkopo.

Njia ya pili ni kwenda ofisi za halmashauri na uombe kupimiwa shamba lako. ..andika barua kwa mkurugenzi, ipitishe kwa mwenyekiti then kata ndipo iende wilayani. ...utaratibu mwingine ndio utafuata, tatizo ni moja procedures zote hizo zinachukua muda mrefu sana kukamilika. ..unless upate mtu wa kukusimamaia kuna urasimu mwingi sana masuala ya ardhi
 
Asante sana Jigoku kwa nondo hizi.., nimepata kitu hapa. nadhani inaweza kuwa rahisi kutafuta hati independent kuliko kupush process za kijiji kizima. Ngoja niendelee kuyaendeleza wakati naendelea kuexplore opportunities za kupata hati ili yaninufaishe zaidi.
 
Kama unahitaji kupata granted right occupancy,ni lazma uhawilishaji ufanyike...yaan kubadil aina ya ardhi kutoka ardhi ya kijiji kuwa ardhi ya kawaida,ambao ni mchakato mgumu wenye hatua nyingi,njia rahisi ni kupata Hati ya kimila ambayo hatua zake ni kama mdau alivyoelekeza hapo juu
 
Dah kuna watu mnajua vitu humu...ila kuongea procedure ni rahisi tu acha uanze sasa uone urasimu wa serikali...hawajui ukipewa hati utalipa ada ambayo ni mapato kwa serikali...asante jigoku kwa nondo...
 
Mie Nina Shamba kiromo pale nyuma ya new kiromo hotel kuna kipindi ulikuwa mradi wa EPZA kwa hawakufika na hata waliowafikia hawajawalipa toka 2009 nilijaribu kufatilia kuhusu upimaji nikaona ardhi bagamoyo na mwenyewe utapeli umekuwa mwingi nilichoamua ni kuendeleza tu labda magufuli akatumbue jipu kule pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…