popah21
Member
- Jun 8, 2023
- 13
- 6
Siasa na utumishi wa uma ni vitu viwili tofauti. Utumishi wa umma ili uwe bora basi jukumu la kutenganisha taaluma za kisiasa na taaluma za mambo ya utumishi wa umma ni muhimu. Tanzania tunatengeneza sera nyingi, ili kuhakikisha zinamsaidia Mtanzania. Nikinukuu maneno ya profesa Mukandala mwaka 2000 aliwahi kusema hvi" je sera tunazotengeneza zina uhalisia na jamii za Kitanzania na Kiafrika kwa ujumla?". Jibu hilo bado mpka leo hii wanasiasa, watu wa masuala ya kijamii wameshndwa kua na jibu sahihi ya sera gani ambazo zitakua halisi za maisha ya Mtanzania na Muafrika kwa ujumla. Hivyo basi kwa sasa ni bado tunahitaji sera au nini tunahitaji kwa Tanzania ya Leo, ya Sasa na ya baadae?. Swali hili limekuja kua gumzo kutokana na changamoto kadha wa kadha wanazopitia Watanzania kwa sasa mfano wa changamoto hizo ni kama zifuatazo.
Kukosekana kwa weledi wa kiutendaji wa masuala mbalimbali yakiwemo ya kijamii, hii imetokana na mabadliko makubwa ya kiteknolojia yanaendelea kushamiri duniani. Hapa je Tanzania tumejiandaa kua na watumishi watakaoendana na mabadliko ya harakat yanayotokea katika ulimwengu wa teknolojia?. Jibu la karibu linaonesha kua bado Tanzania hatujajiandaa na mabadliko hayo, hivyo tunahitaji Tanzania itakayokua na wasomi, wanachuoni na watumishi katika kada mbalimbali zikiwemo kada za umma watakaoweza kutumia teknolojia katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku, hii itapelekea kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika shughuli zote. Mathalani, endapo tutatengeneza sera ya mabadiliko ya mafunzo katika elimu za juu kwa kuanzisha somo la teknolojia kua ni la kazima kwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza kama ilivyo kwa masomo kama vile masomo ya maendeleo itasaidia kwa kiasi kikubwa kua na watumishi wenye uelewa wa hali ya juu juu ya matumizi sahihi ya teknolojia, mfano hivi karibuni kumekua na ulalamishi kua wanafunzi wengi wanapokua katika mafunzo yao(Field) wnapopewa kompyuta watumie wengi wao hushindwa kutumia teknolojia kuingiza taarifa mbalimbali kwenye kompyuta hivyo endapo tutaangalia sehemu hii ipasavyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia Tanzania ya matamanio ambayo kila siku tunaiota.
Uwepo wa bajeti ndogo katika sekta mbalimbali, Serikali inatenga fedha kwa ajili ya sekta mbalimbali, Lakini je hizo fedha zinazotengwa ni toshelezi kuendana na mahitaji ya watu, mfano je bajeti ya fedha ya mwaka 2023/2024 ni toshelezi? Hapa tunakuja kugundua kua bajeti bado si toshelezi na hii imejidhihirisha katika nyanja mbalimbali, mfano ruzuku iliyotengwa kwa mwaka 2023/2024 mwaka wa fedha, ilionesha dhahiri kua serikali haiwezi kupambana na changamoto za ghafla ambazo zinatokea katika jamii, mfano mfumuko wa bei ya sukari na mafuta, Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanathibitisha kua ili nchi iwe katika uchumi wa kati basi nchi hiyo haina budi kua na bajeti ambayo itawezesha kutatua matatizo ya kidharura mfano mfumuko wa bei na madhara mengine kama vile kimbunga. Nchi yetu bado ipo nyuma sana katika kutenga ruzuku ya kukidhi matatizo yote haya, hivyo ili tuifikie Tanzania tunayoitaka haina budi kufanya mabadliko ya sera katika masuala mazima ya bajeti, na kueka ulazima ambao utamlazimisha waziri wa fedha kutoa fedha wakati wowote panapokua na matatizo makubwa ambayo yanayoathiri jamii.
Pia tatizo jengine ni tatizo la miundombinu mibovu na isiyokidhi kiwango hali inayopelekea kukwama kwa masuala mbalimbali ya kiuchumi, na kijamii. Mfano maeneo mengi ya vijijini TARURA wameshindwa kutengeneza Barbara bora zenye kiwango cha lami ambazo zingewezesha shughuli za kiuchumi na hatimaye kuchangia maendeleo ya Taifa. Kama Taifa tunahitaji Tanzania itakayokua na miundombinu sahihi itakayoweza kupitika muda wote na katika nyakati zozote, mfano kipindi cha mvua barabara ziweze kupitika bila kuharibika, madaraja yawe imara na mengine mengi. Kwahyo ili TARURA waweze kufanya hvi katika miji na wilaya nyingi zilizopo Tanzania haja ya kubadilisha sera ya kiutendaji ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 inahitajika kua ni suala la muhimu na kuliendea kwa harakat, Mamlaka za miji zinatakiwa zipewe Mamlaka kamili ya kuendesha na kupanga bajeti zake pasi na kuomba idhini au rufaa kutoka Serikali kuu au kwa waziri mwenye dhamana, Mamlaka za Serikali za mitaa ndiyo zinataarifa kamili wapi kunahitaji nini na wapi nini hakihitajiki kwahiyo kutekezwa kwa ujenzi wa miundombinu na Serikali kuu ni suala ambalo linakwamisha maendeleo thabiti ya Tanzania, kwahiyo ili tuifikie Tanzania tunayoitaka kwa miaka mitano zaidi mbele hizi Serikali za mitaa zinatakiwa kupewa Mamlaka ya kutosha ili zifanye kazi kiufanisi na kuchagiza maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Zipo changamoto nyingi mno, ila kikubwa kinachohotajika ili tuifikie Tanzania tunayoitaka kwa miaka mitano zaidi mbele ni mabadiliko ya kisera, William Ruto aliwahi kusema" hatupo ili tutii Sheria, Bali Sheria zipo ili zitusaidie na kama hazitusaidii basi tuzibadilishe" kauli yake haipo mbali sana na nini ambacho tunakihitaji kwa Tanzania yetu ya baadaye. Hivyo ni jukumu la mamlaka husika kuangalia na kufanya upembuzi yakinifu kwa sera mbalimbali na kufanya mapitio ya sera kwamishi na endapo wakibaini changamoto basi hatua za kiutatuzi zichukuliwe maramoja, hapa tumejadili kwa uchache sera ambazo ni kwamishi, Lakini zipo sera nyingi mno, asasi za kiraia zinatakiwa zifanye kazi katika eneo hili kama walivyofanya mnamo mwaka 2019 wakati Serikali inafanya mabadiliko madogo katika sera ya vyombo vya habari, Jamii Forum kama asasi iliibua changamoto hii na kuzifanya taasisi mbalimbali kufatilia juu ya uhuru wa vyombo vga habari, hivyo katika mitizamo ya kisiasa na utumishi wa umma Tanzania tunayoitaka na kuiota haitokuja pasi na mabadiliko ya kisera Aidha mabadiliko madogo madogo au hata mabadiliko makubwa ya sera kamili. Sera ni Sheria.

Upvote
3