Alisema atappoint mtu kulingana na uwezo wake , uadilifu , na uchapakazi wake akitanguliza maslahi ya umma kwanza. Viongozi wa Mashirika ya Umma kama vile NHC, PPF, NSSF, TANESCO, TANAPA , AICC na mengineyo watachaguliwa kwa vigezo vitakavyowekwa sio uswahiba. Mashirika haya yamekuwa yakiendeshwa kibabe babe na kuwanyima wananchi haki . Mfano NHC inayodeal na nyymba za kuishi.Siku hizi wamekuja na sera za kibishara wakasahau madhumuni ya kuanzishwa kwake hivyo kuwafanya wapangaji wajipinde sana na mwisho wa siku Wahindi tu ndio wanafaidi.Hii haikubaliki. Wengine wamekuwa wakitoa fedha kufadhili ccm na viongozi wake kinyume na sheria. Haya yote yatakwisha.
Nyumba bora ni pamoja na sera bora za nyumba ikiwemo nyumba za kupangisha.Sio Mwenye nyumba acharge kodi kwa dola wakati hatuna dola .