Hatimae mh. Jenista Mhagama anena kuhusu ajira za walimu wapya

CALMAN

Senior Member
Joined
May 23, 2013
Posts
190
Reaction score
54
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia kutoka kwa wakuu wa shule waliokuwa na kikao na Naibu waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi hapo juzi Mkoani Iringa, mhe. Jennista Muhagama naibu wa wizara hiyo alionekana kuwasihi sana wakuu hao wa shule kuwa wavumilivu na moyo wa subira kwa upungufu wa walimu uliopo na kuahidi ahadi iliyokuwa na mashaka ndani yake kuwa, nanukuu "labda ajira mpya za walimu zitatoka April mosi" kutokana na ukosefu wa fedha za malipo kwaajiri ya walimu hao wa ajira mpya kwa kuwa serikali imeelekeza fedha nyingi kwenye malipo ya utekelezaji wa programu ya BRN na fedha nyingine zitatumika kwa malipo wa wajumbe wa bunge la katiba.


Kwa mtazamo huu naitafakari serikali nakuiona ni yakusadikika kwa kushindwa kutumia kila fungu la fedha kulingana na wizara husika, lakini pia mhe Majaliwa TAMISEMI kama kiongozi aliuhadaa umma kwa kutosema ukweli na kudanganya kuwa ajira zitatoka mapema january kwa kuajiri walimu 26,000 wa shule za msingi na sekondari hii ni taarifa yake akiwa Morogoro na Maafisa Elimu. Wahanga wa ajira mpya tunapaswa kuchukua hatua kuelekea Ofisi za wizara ya Elimu Dsm nipo tayari kuongoza maandamano hayo tuwasiliane kupitia namba +255 682 893 290

------------------------


 
Inakera msomi kukaa unasubiria ajira serikalini baadala ya kujipanga kwa kujiajiri.
 
inakera sana lakini wazo la kusema wahanga wa ajira mpya waandamane kwenda wizarani siliungi mkono
 
vuteni subira mtaajiriwa tu maandamano si suluhu ya tatizo hilo.sina uhakika kama kuna haki ya mhitimu kuajiriwa na serikali vinginevyo migomo ingekuwa kila siku!¡!!!!!!!!!!
 
Acha uongo Mr,wakuu wa shule ndio wapewe taarifa embu toa nonsense zko
 
serikali mbona mnashinswa kutoa ajira kwa walimu toka mwaka jana hadi leo........................ ? Wengi walimu walijua leo nd' siku nzuri kwao kumbe sivyo jamani mwenye fununu yoyote tujuze baxi
 
Taarifa nlizozipata kutoka kwenye chanzo mwaka huu walimu wa sayansi na hesabu ndo watakao ajiriwa tu wamasomo ya arts mpaka budget ipite yaani mwezi wa 7
 
Muandamane kwani kuna mkataba mliingia na serikali kuwa mkimaliza mnaajiriwa.
 
jamb mbona unakatisha watu tamb ya kuajiriwa!
 
Inakera msomi kukaa unasubiria ajira serikalini baadala ya kujipanga kwa kujiajiri.

Kwa taaluma aliyoisomea(ualimu) we unafkr angejiajirije labda? afungue tuition center? apige tempo? "tumejenga tabia kisha tabia zikatujenga"
 
Ngumu kumeza Mkuu!!! Lakini ikumbukwe Mukulu alisema 'mapema mwakani', kwa hiyo hata mwezi wa 5 bado itakuwa mapema.
Nipo kaka, nnaitafakari hii taarifa....................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…