Hatimae na mimi nimekaona huku!

General Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2015
Posts
1,868
Reaction score
2,210
Habarini za j3 ILIYOTUKUKA waheshimiwa sana wana jamvi,nashangaa hii siku watu wanaiita eti blue Monday hata sijui kwanini haikuwa red Monday, black Monday au green Monday.....ok hata ivo hilo sio lililonileta kwa dharula hapa jukwaani.....

Kumekuwa na ongezeko la watu wanauvumbua miti inayotaka kufanana na taswira za viongozi mbali mbali.....kuna ile ya mwembe unaofanana na JK wa kwanza.....kuna nyingine ya mti unaotaka kufanana na Don Trump.....na mimi huku nilipo sasa kwny shughuli zangu nimebahatika kuona ka mti flani hivi kanafanana sana na taswira ya JK wa pili...!!

Ziara ya shughuli zangu bado inaendelea, wiki ijayo nitakuwa kigoma naamini huko nitaona ka mti kenye taswira ya kufanana na JPM nikienda bukoba ckosi kuona mti au mgomba wenye taswira ya Gaddafi,pale shinyanga naweza kukuta mti una taswira ya Idd Amin.....nk. nk.

Nitaendelea kuwajuza tu, pia kwa mlioko mjini nawatakia maandalizi mema ya ujenzi tarehe 1 September, lakini unapotoka nyumbani kwenda kwny huo ujenzi hakikisha unaandika mirathi kabisa kwa familia yako ili baadae isije kuleta tabu kwa watoto kugombea mirathi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…