Hatimae ngalangala (Noah Voxy) nimeliuza

MIGUGO

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
2,137
Reaction score
3,931
Baada ya kuhangaika na Noah voxy ambalo kwa muonekano wa nje linaonekana jipya (pamba) au wanasemaga in mint condition ila ilitaka kunifirisi.

Jamaa wamenipatia mil 6.5 inanitosha kabisa maana leo imehiti kesho gear box mara izime ghafla mara nozzle kesho throttle.

Ilishawahi nitia Aibu niko na wakwe vioo havipandi wala kushuka huku mvua inanyesha.Walinuna wakawa wananiteta kilugha.

Kuna siku ilinuka petrol ndani gari mzee akaniambia unataka kunifanya ya kibwetele mwanangu. Baadae ndio nikaelewa.

Aisee Noah!!!
 
Niliwahi kununua Noah new model kutoka Japan, injin ilikuja vipande vipande... Clearing agent naye akapoteza document.. Gari ilikaa bandarini miezi mitano.. Nilipofanikiwa kulitoa, nikaliuza faster!
 
Nilikuwa naipenda mno service siruki km.Yaani unakuta unaamka asubuhi tatizo flani linaanza ghafla.
Kawaida hiyo kwenye magari. Kilichotokea ni kwamba ulinunua gari bila kulifanyia analysis kubwa ya kila kitu wakati lilikuwa limeshazeeka.
Mie nikinunua gari used say nimeagiza kama ni Toyota lazima nilipeleke Toyota Tanzania wakalicheki na kuliweka sawa ndio naanza kulitumia. Wengi hawafanyi hivyo wanachojua ni kumwaga oil na kubadilisha filter tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…