The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Hatimae Serikali imeanza kutoka kwenye zama za ujinga za kutenga shule kadhaa na kuziita za vipaji maalumu.
Serikali kusitisha mfumo wa kutangaza mwanafunzi wa kwanza sijui wa mwisho ni mwanzo mwema wa kuhama kutoka kwenye ujinga/zama za giza na kwenda kwenye mwanga na kuleta mapinduzi kwenye mfumo wetu wa elimu.
Wewe mtoto mmoja anasoma Kitopeni secondary school ambako hakuna walimu wala miundombinu ya kutosha ya kujifunzia, mwingine anasoma Feza ambako kuna kila miundombinu ya kujifunza, halafu uwape mtihani sawa halafu useme wa Feza ana kipaji maalumu na yule wa kitopeni hana kipaji chochote, ni zero brain, hakuna kitu.
Kwa mfumo wetu hata ukiiba mitihani ukapata A masomo yote wewe una kipaji maalumu.
Nimefurahi kuona Serikali inaanza kufanya kazi, kuanza kubadilisha mfumo wetu wa elimu uliopitwa na wakati.