mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,707
Wadau nadhani yaliyotokea Misri kwa Timu ya Taifa sote ni Mashahidi.Timu imecheza mechi 3 ,imefungwa jumla ya magoli 8-2 na kuwa ya mwisho ktk kundi lake na kisha kutupwa nje ya mashindano raundi ya kwanza.Kocha Amunike tayari kajitetea kuwa ni kukosa uzoefu.Wadau tulisema mapema mara baada ya timu kufuzu Afcon kuwa mazoezi ya kuwajengea uwezo na uzoefu wachezaji yaanze lakini TFF haikutaka matokeo yake ikapeleka timu Misri siku 10 kabla eti ikafanye mazoezi hakika TFF imevuna ilichopanda.Watanzania tuache siasa kwenye mpira, ndio maana hata FIFA haitaki siasa eti Taifa Stars ni timu ya CCM,eti inatekeleza Ilani ya CCM.